Amani iwe juu ya Jua la utakasifu na bibi wa tabia njema, amani iwe juu ya mama wa wachamungu bibi mtakasifu Fatuma Zaharaa bint Muhammad bun Abdullah na Khadija Kubra (a.s) katika siku ya kufariki kwake kishahidi.
Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) aliishi katika zama zenye mitihani ya kitabligh ya ujumbe wa Mwenyezi Mungu toka utoto wake, alizingirwa pamoja na wazazi wake (baba na mama) pamoja na ndugu wengine wa bani Hashim katika shamba la Abuu Twalib akiwa na umri wa miaka miwili tu.
Mzingiro uliisha baada ya miaka mitatu ya dhiki, kisha akapata mtihani wa kufiwa na mama yake kipenzi na Ammi wa baba yake akiwa mwanzoni mwa mwaka wa sita katika umri wake, akaishi pamoja na baba yake katika kipindi kigumu kilicho jaa matatizo mengi, akawa liwazo lake wa pekee kutokana na visa alivyo kua akifanyiwa na makafiri wa kikuraishi.
Alihama pamoja na mtoto wa Ammi yake akiwa na wakina Fatuma wengine, kwenda Madina akiwa na miaka nane, akaendelea kuishi pamoja na baba yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), hadi alipo olewa na Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) na kutengeneza nyumba bora zaidi katika uislamu baada ya nyumba ya Mtume (s.a.w.w), nyumba takasifu inayo tokana na mtoto mtakasifu na Kauthar ya kizazi cha Mtume (s.a.w.w).
Bibi Fatuma (a.s) akiwa katika ndoa na Imamu Ali (a.s) aliwazaa mabwana wa vijana wa peponi, watoto wa Mtume (s.a.w.w) Hassan na Hussein maimamu wawili watukufu, na mabinti wawili watukufu bibi Zainabu Kubra na Ummu Kulthum wapiganaji wenye subira, na ujauzito wa tano ukaharibika wa mtoto ambaye angeitwa Muhsin, baada ya kufariki kwa baba yake, katika tukio la kushambuliwa nyumba yake (nyumba ya utume), akawa mtoto wa kwanza kufishwa na mama huyu mpiganaji baada ya kufariki kwa baba yake kwa ajili ya kulinda ujumbe wa baba yake usipotoshwe na kuharibiwa.
Alikua pamoja na baba yake na akawa pamoja na mme wake katika mazingira magumu, akaunusuru uislamu kwa juhudi zake na jihadi yake pamoja na ufaswaha wake sambamba na malezi yake kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) alio waachia jukumu la kunusuru uislamu baada ya kufariki kwake, akawa mtu wa kwanza katika watu wa nyumba ya Mtume kuungana nae, akawa kielelezo cha ushujaa, subira na kujitolea muhanga, na akafika daraja la juu kabisa na kuwazidi watukufu wa mwanzo na wa mwisho, katika kipindi kifupi kapisa ambacho ni vigumu kwa mwanadamu kufikia utukufu na ukamilifu alio kua nao.
Mtume (s.a.w.w) anasema katika hadithi kua: (Hakika Mwenyezi Mungu anachukia kwa kuchukia Fatuma na anaridhia kwa ridhaa yake).
(Fatuma ni pande la nyama itokanayo na mimi, atakae muudhi kaniudhi mimi na atakae mpenda kanipenda mimi)
(Fatuma ni roho yangu na moyo wangu uliopo katikati ya mbavu zangu).
(Fatuma ni mmbora wa wanawake wa ulimwenguni).
Bila shaka kifo cha bibi Zaharaa (a.s) kilitokea mwaka wa kumi na moja hijiriyya, kwani Mtume (s.a.w.w) alifanya hija ya mwisho (wida’a) mwaka wa kumi, na akafa mwanzoni mwa mwaka wa kumi na moja, wanahistoria wamekubaliana kua bibi Fatuma aliishi chini ya mwaka mmoja baada ya kufariki baba yake, fahamu kua alikua msichana mwenye afya nzuri wakati wa uhai wa baba yake, imepokewa kua aliishi miezi sita baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), na ikapokewa kua aliishi siku tisini na tano, na ikapokewa kua aliishi siku sabini na tano au chini ya hizo.
Kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Hakika (bibi Fatuma a.s) alifariki katika mwezi tatu Jamadal-Aakhar mwaka wa kumi na moja hijiriyya).
Kutoka kwa Imamu Baaqir (a.s) anasema: (Bibi Fatuma a.s) alifariki akiwa na umri wa miaka kumi na nane na siku sabini na tano).
Abuu Farji Isfahani anasema kua: bibi Fatuma Zaharaa (a.s) alifariki baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w) kwa kipindi ambacho watu wametofautiana, wenye kusema muda mrefu wanasema miezi sita, na wenye kusema muda mfupi wanasema siku arubaini, uhakika katika hili ni riwaya ya Imamu Baaqir (a.s), inayo sema kua alifariki baada ya miezi mitatu toka kufariki kwa Mtume mtukufu.
Amani iwe juu yake siku aliyo zaliwa, na siku aliyo kufa kishahidi, na siku atakayo fufuliwa kua hai akiwa na mikono ya Abulfadhil Abbasi (a.s) aliyo katwa wakati akipigana kumhami mbora wa mashahidi Imamu Hussein (a.s).