Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanaita: Mwenyezi Mungu ayakuze malipo yako Sayyidy yaa Hussein kwa kifo cha mama yako Zaharaa (a.s)…

Maoni katika picha
Khudaam kamar ya Hussein khudaam kamar *** Swarkhata mina nahri ya Hussein khudaam kamar.

Kutoka kwa Abbasi mshirika wake na bendera yake na utukufu wake *** kutoka kwa mshauri na uti wake wa mgongo.

Zaharaa ana athari ewe Hussein Zaharaa ana athari *** kutoka katika kipindi kibaya ewe Hussein kutoka katika kipindi kibaya.

Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wapaza sauti zao wakiimba maneno hayo ya kuomboleza na mengineyo, huku macho yao yakitokwa machozi na nyoyo zao kujaa huzuni, wakikumbuka shahada ya mtoto wa Mtume Mtukufu bibi Fatuma Zaharaa (a.s), watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) walijipanga na kuelekea katika kaburi la Imamu Hussein (a.s) kutoa taazia kufuatia kifo cha mama yake (a.s), huku wakikumbuka tukio linalo umiza roho za wapenzi wa Ahlulbait (a.s) na wafuasi wao katika siku kama hizi, wakapokelewa kwa beti za huzuni kutoka kwa watumishi wa Imamu Hussein (a.s), kisha wakafanya majlisi ya kuomboleza ya pamoja katika ukumbi wa haram tukufu.

Kumbuka kua siku kama hizi katika kila mwaka huzungumziwa shahada (kifo) cha Swidiqah Fatuma Zaharaa (a.s), siku za kuadhimisha kifo chake zimetofautiana kutokana na kutofautiana kwa kauli zinazo zungumzia kifo hicho, ambapo kuna kauli tatu mashuhuri zaidi, ambazo hufanywa kumbukumbu za huzuni kwa mujibu wa kauli hizo, na vipindi hivyo huitwa misimu ya huzuni za Fatwimiyya, ambazo ni:

Kauli ya kwanza: Mwezi 8 Rabiu-Thani, kwa mujibu wa riwaya ya kuishi kwake baada ya baba yake Mtume (s.a.w.w) siku 40, na huitwa (Msimu wa kwanza wa Fatwimiyya).

Kauli ya pili: Mwezi 13 Jamadal-Ula, kwa mujibu wa riwaya ya kuishi kwake baada ya baba yake Mtume (s.a.w.w) siku 75, na huitwa (Msimu wa pili wa Fatwimiyya).

Kauli ya tatu: Mwezi 3 Jamadal-Aakhar, kwa mujibu wa riwaya ya kuishi kwake baada ya baba yake Mtume (s.a.w.w) siku 95, na huitwa (Msimu wa tatu wa Fatwimiyya).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: