Maoni katika picha
Shughuli ya kutoa huduma imeanza kufuatia kumbukumbu ya shahada ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili ambapo tupo ndani ya siku hizo, na huitwa msimu wa pili wa huzuni za Fatwimiyya, utawaona wanashindana kutoa huduma hii ndogo yenye maana kubwa, utaona mazuwaru wanasimama katika meza hii kwa ajili ya kunywa chai wanayo pewa na mikono mitukufu ya maalawiyya jirani na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi hii pamoja na udogo wake lakini ina mwitikio mkubwa, kwa sababu inafanywa karibu na sehemu takatifu, watoa huduma ni masayyid ambao ni watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na baadhi ya watu wa kujitolea kutoka nje ya Ataba, mazuwaru huja rasmi kunywa chai wanayo karibishwa na kupewa na maalawiyya.
Kumbuka kua miongoni mwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kuna masayyid, wapo chini ya idara inayo fungamana na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu inayo itwa (Idara ya masayyid watumishi), idara hiyo ina majukumu mengi, na kipindi cha ziara maalumu au tarehe za kufariki kwa maimamu (a.s) majumu yao huongezeka zaidi, na miongoni mwa matukio ambayo huyaadhimisha rasmi ni tukio la kumbukumbu ya shahada ya Zaharaa (a.s), wanaratiba maalumu ya kuhuisha tukio hili, hufanya majlisi za maombolezo na hushiriki katika mawakibu za kuomboleza na hufanya kazi ya kutoa huduma kwa mazuwaru, hivyo wakati fulani utawakuta ndani ya uwanja wa haram tukufu na wakati mwingine utawakuta nje wakiwa wamevaa sare zao ambazo humfanya zaairu kua na utulivu wa roho zaidi.