Maukibu ya wanawake ni miongoni mwa harakati za msimu wa huzuni za Fatwimiyya, yatoa taazia kwa maimamu watakasifu katika kumbukumbu ya kifo cha Zaharaa (a.s)…

Maoni katika picha
Malaika wa mbinguni walipata huzuni na uchungu kutokana na kuvunjika kwa mbavu zako ewe Swidiqah, hakuna furaha tena iliyo ingia katika nyumba ya Mtume baada ya kukukosa, maombolezo yaliyo jaa simanzi na huzuni, maukibu ya wanawake imefanya matembezi ya huzuni za Fatwimiyya chini ya usimamizi wa kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), wakitoa taazia kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukumbu ya kifo cha Swidiqah Fatuma Zaharaa (a.s).

Maukibu hiyo imeundwa na kundi la wakina mama wenye majina ya Fatuma wanao fuata mwenendo wa bibi Fatuma Zaharaa mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), walitembea huku wakiwa wametanguliwa na watumishi ambao ni masayyid pamoja na kundi la watoto waliovaa nguo zinazo ashiria huzuni, kituo chao cha kwanza kilikua ni katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha wakaelekea katika uwanja wa katikati ya haram mbili huku wakiimba kaswida za kuomboleza, wakaenda hadi katika haram ya Bwana wa mashahidi Abu Abdilahi Hussein (a.s) na wakampa pole kwa kufariki mama yake bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Kumbuka kua kongamano la siku za Fatwimiyya kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu bwana Riyadh Ni’mat Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Ni kongamano la kitamaduni linalo simamiwa na kitengo chetu, huchukua siku kumi, hua na program nyingi za maombolezo, baadhi ya program hizo ni kuangazia hatua za uhai wa bibi Zaharaa (a.s), hapo awali program hizo zilikua zinafanywa siku moja tu, kwa kua bibi Zaharaa (a.s) anastahiki zaidi ya haya, tumejalia tukio la kukumbuka kifo chake sawa na tukio la Ashura, na vyovyote tutakavyo fanya hatuwezi kufikia stahiki yake (a.s), tunatarajia kufanywa kwa program hizi kunasaidia kuangazia baadhi ya dhulma alizo fanyiwa (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: