Kufuatia kipindi cha likizo: Idara ya maktaba ya wanawake yaendesha mradi wa marafiki wa maktaba na wana utamaduni…

Maoni katika picha
Ikiwa ni muendelezo wa miradi ya kielimu na kutaka kunufaika na kipindi cha likizo, idara ya maktaba ya wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendesha mradi wa (Marafiki wa maktaba na wana utamaduni), unao lenga wanafunzi wa kike katika kipindi cha likizo kuanzia (01/02/2018m) hadi (15/02/2018m).

Mradi huu unatokana na ukweli kua; kusoma ndio njia kuu ya kukuza akili na kuipatia elimu mbalimbali, na baada ya kuwepo kwa utitiri wa mitandao ya kisasa ya mawasiliano ambayo inawashughulisha sana vijana, hivyo Atabatu Abbasiyya tukufu imeona vizuri kuandaa mradi huu utakao saidia wanafunzi waweze kujisomea kwa utaratibu maalum, na watakua na mashindano pamoja na kutoa zawadi kwa watakao fanya vizuri, itasaidia kumfanya kila mshiriki kua (Rafiki wa maktaba) na kuyafanyia kazi anayo soma kwa kuandika (muhtasari, kuchora, kisa au shairi) mradi huu unahusisha wanafunzi wa:

  • 1- Shule za Ameed (Sekondari ya wasichana Al-Ameed) kwa kuwasiliana na kitengo cha maelekezo ya kimalezi.
  • 2- Shule za wasichana za Alkafeel katika mkoa wa Karbala na mikoa mingine.

Kwa maelezo zaidi au kushiriki, unaweza kutembelea ofisi ya maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: