Maoni katika picha
Ratiba hiyo inatekelezwa kwa ajili ya kujenga uwelewa wa msimu wa huzuni za Fatwimiyya kwa wanafunzi wa shule za Ameed, ambapo wanafunzi walio shiriki wametoka katika shule za (Shule ya msingi ya wasichana Al-Ameed, Shule ya msingi ya wavulana Al-Ameed, Shule ya msingi ya wasichana Al-Qamaru, Shule ya msingi ya wavulana Saaqi, Shule ya msingi ya wavulana Sayyidul-Maa na Shule ya msingi ya wavulana Nurul-Ameed).
Katika program ya uchoraji wameshiriki zaidi ya wanafunzi thelathini na tano wavulana na wasichana kutoka katika shule za Ameed, kama sehemu ya kukumbuka dhulma alizo fanyiwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) ambapo wamechora moja kwa moja (live) katika karatasi.
Katika msimu huu wa huzuni za Fatwimiyya unao simamiwa na kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu kwa muda wa siku kumi kunahusisha vitu vingi, ikiwa ni pamoja na (Panorama) kutengeneza sauti na picha za riwaya zinazo elezea kisa cha kudhulumiwa kwake (a.s) na tamasha la uchoraji kwa watoto walio chini ya miaka kumi pamoja na majlisi za kuomboleza na vitu vingine.