Ofisi ya maonyesho ya kimataifa ya vitabu Karbala awamu ya kumi na nne, ambayo hufanyika pembezoni mwa kongamano la kimataifa na kitamaduni Rabiu Shahada litakalo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo (Kwa utukufu wa Hussein (a.s) tumepigana na kwa utukufu wa fatwa tumeshinda), imetangaza kuanza kwa usajili wa washiriki wa maonyesho hayo, na wametoa wito kwa taasisi za kielimu na vituo vya usambazaji vya kimataifa, kiarabu na vya hapa Iraq pamoja na maktaba za kielimu na kibinadamu watakao penda kushiriki katika tukio hili la kitamaduni, na kuonyesha vitabu wanavyo chapisha kwa ajili ya kubadilishana uzowefu na kuingiza vitabu vipya sokoni.
Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea mtandao ufuatao:
https://rabee.alkafeel.net/index.php?main
au unaweza kuwasiliana nasi kwa barua pepe: rabee@alkafeel.net au kbfair@alkafeel.net.
Au piga simu namba: +9647703713186.
Kumbuka kua ofisi ya maonyesho imeweka kipindi maalumu cha kupokea maombi ya kushiriki, na maonyesho yataanza (28 Rajabu 1439h hadi tarehe 8 Shabani) sawa na (15/04/2018 – 25/04/2018m).