Kitengo cha habari na utamaduni chaweka hema la mafunzo kwa wanafunzi wa chuo cha Alkafeel…

Maoni katika picha
Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya elimu na ubunifu, kimeweka hema la mafunzo kwa wanafunzi wa chuo cha Alkafeel iliyopo chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kuhakikisha wananufaika na kipindi cha likizo, na kuwaongezea elimu na maarifa, sambamba na kulea vipaji vya wanafunzi kielimu na kivitendo, ili viwasaidie katika maisha ya nyumbani na shuleni. Kiongozi wa idara ya elimu na ubunifu Ustadh Ridhwan Salami ameeleza kuhusu hema hili kua: “Hema hili ni miongoni mwa shughuli zinazo simamiwa na kuendeshwa na kitengo cha habari na utamaduni, ofisi yetu imeandaa ratiba inayo endana na viwango vya wanafunzi chini ya usimamizi wa kamati ya wataalamu, ratiba hizo zina vipengele vingi vinavyo changia kuboresha uwezo wa mwanafunzi kiakili na kifikra, na kwa upande mwingine ratiba hizi zinawafanya wawe na ukaribu na malalo matakatifu ambayo yamekua moja ya vituo muhimu kielimu na kiutamaduni, kutokana na kufanya shughuli mbalimbali katika sekta tofauti”.

Akaongeza kusema kua: Ratiba hii ni ya siku saba, inahusisha mambo yafuatayo:

  • - Kutembelea Ataba tukufu za (Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya, Askariyya na Abbasiyya) pamoja na kukagua baadhi ya miradi ya Ataba hizo tukufu.
  • - Mihadhara ya kuwajengea uwezo itakayo tolewa na wakufunzi wa kimataifa kuhusu mada mbalimbali.
  • - Ratiba ya mapumziko kwa kutembelea maoneo ya kitalii na mengineyo.

Dokta Amjadi Rasul Awadi ambaye ni kiongozi katika chuo cha Alkafeel na aliye kua msimamizi wa hema la Skaut, amebainisha kua: “Katika ratiba hii wameshiriki zaidi ya wanafunzi (80) kutoka vitengo tofauti, hakika hii ni fursa nzuri, kuwakaribisha wanafunzi hawa katika eneo hili takatifu, wala sio jambo geni kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kufanya program ya aina hii, kutokana na namna inavyo jali tabaka hili muhimu katika jamii, inafanya kila iwezalo kuhakikisha inatoa malezi bora kwa wanafunzi kielimu na kiimani, ili kuwawezesha kupambana na changamoto wanazo kutana nazo, ratiba ina mambo mbalimbali yanayo wasilishwa kwa njia nyepesi na rahisi inayo endana na akili za wanafunzi ili kuwavutia na kuwafanya waelewe zaidi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: