Kwa uthibitisho na kwa hati ya mkono wake na muhuri wake mtukufu: Marjaa dini mkuu atoa ujumbe maalum kwa mashahidi wa fatwa…

Maoni katika picha
Mtandao wa kimataifa Alkafeel umepata barua iliyo andikwa na Marjaa dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani inayo husu familia za mashahidi wa fatwa tukufu ya kujilinda.

Limefanyika hili wakati ambao Atabatu Abbasiyya tukufu inamradi unao lenga kusaidia familia zote za mashahidi wa fatwa ya kujilinda.

Mheshimiwa Marjaa dini mkuu anataka kuwe na uangalizi maalumu kwa familia za mashahidi, ameandika kwa mkono wake ujumbe unao onyesha umuhimu wa jambo hilo na kawaombea dua.

Mtandao wa Alkafeel umepata nakala, na haya ndio yaliyomo katika ujumbe huo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu.

“Hakika waliopata shahada katika vita ya jihadi ya kujilinda wana haki kubwa kwetu sote, na wana daraja kubwa, namuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awafufue pamoja na answari wa Hussein (a.s)”.

-------------------------------- Sayyid Ali Husseini Sistani
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: