Maoni katika picha
Mkuu wa chuo Dokta Nuris Muhammad Dahaan na msaidizi wa rais wa kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri walitoa zawadi kwa mshiriki huyo kama sehemu ya kumpongeza kwa ushindi alio pata yeye kwanza kama mtu binafsi, na kitengo cha lugha katika kituo cha Maahadi ya Alkafeel cha kutoa elimu na kukuza vipaji ambacho kimepiga hatua kubwa katika sekta ya elimu kwa kufikia ufaulishaji wa %100.
Mkuu wa idara ya lugha katika chuo cha Alkafeel Ustadh Mahmuud Swabbaar amesema kua, idara yao inaendelea kutoa kozi hizi na watajitahidi kuongeza lugha zingine, akatangaza kua matokeo ya mtihani wa mwisho yameonyesha kufaulu wanafunzi wote walio shiriki kwa asilimia %100, hii ni mara ya tatu kupata matokeo kama haya.
Fahamu kua Maahadi ya Alkafeel ya utoaji wa elimu na kukuza vipaji iliyopo chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ni moja ya vituo muhimu katika ufundishaji wa lugha, huendesha kozi za lugha ya kifarisi katika mkoa mtukufu wa Karbala, na wamesha hitimu watu wengi tena kwa kupata ufaulu wa juu.
Kumbuka kua washiriki wamesoma kwa muda wa miezi sita sawa na saa (512) za masomo, washiriki hupewa vifaa vyote muhimu katika kujifundisha lugha, kisha hutunukiwa vyeti vinavyo tambulika, fahamu kua idara ya lugha ndio muwakilishi pekee mwenye kibali cha kufundisha lugha ya kifarisi katika shule za sekula, na kutoa mitihani (ya kifarisi) katika mikoa yote ya Iraq, kutoka katika kituo cha kimataifa cha kufundisha lugha ya kifarisi kwa wasio ijua kilichopo katika chuo kikuu cha Firdausi huko Mashhadi.