Kupitia tawi la Landan: Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya nadwa kuhusu visomo vya Qur’an katika kitabu cha Albayaan cha Imamu Khui (q.s)…

Maoni katika picha
Kufuatia mwaliko wa chuo kikuu cha kimataifa cha masomo ya kiislamu katika mji mkuu wa Uingereza Landan, Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya kupitia tawi lake lililopo huko (Landan) wamefanya nadwa ya Qur’an waliyo ipa jina la (Visomo vya Qur’an katika kitabu cha Albayaan cha Imamu Khui), mtoa mada katika nadwa hiyo alikua ni Shekh Dhiyaau-Dini Aali Majidi Zubaidi mkuu wa kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha katika Ataba tukufu, nadwa iliyopata mwitikio mkubwa kutoka kwa wasomi wa dini na sekula pamoja na wapenzi wa Qur’an wa ndani na nje ya chuo.

Nadwa hii ni miongoni mwa mfululizo wa nadwa zinazo fanywa na chuo hiki chini ya kitengo cha masomo ya juu, hualikwa wasomi wakubwa wa Qur’an kwa ajili ya kuja kufafanua moja ya jambo muhimu ndani ya Qur’an tukufu, miongoni mwa mambo hayo ni hili la visomo vya Qur’an, lililo fafanuliwa katika kitabu cha (Albayanu fi tafsiril-Qur’an) cha Imamu Khui (q.s).

Shekh Zubaidi alifafanua mada na akatoa nafasi ya kuuliza maswali na kutoa maoni kuhusu mada hiyo kwa washiriki, naye alijibu maswali na kufafanua mambo yaliyo hitajia ufafanuzi zaidi, washiriki walitoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na juhudi kubwa wanazo fanya kuhusu Qur’an, hadi leo Qur’an imekua na nafasi kubwa sana katika jiji la Landan.

Kumbuka kua lengo kuu la kufunguliwa kwa tawi la Maahadi ya Qur’an tukufu katika mji mkuu wa Landan, ni kutoa elimu kuhusu masomo ya Qur’an kwa mujibu wa mwenendo wa Ahlulbait (a.s), na kukifanya kua kimbilio katika mambo ya Qur’an sambamba na matawi mengine ya Maahadi yaliyopo katika mikoa ya Iraq, na kua mwanzo mwema katika kuanzisha utaratibu wa kufungua matawi mengine nje ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: