Skaut ya Alkafeel yaendesha ratiba ya Rabiu Maarifa ya pili kwa ajili ya vijana…

Maoni katika picha
Kufuatia kipindi cha likizo; Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendesha ratiba ya (Rabiu Maarifa ya pili) yenye anuani isemayo (Raihaanatu Rasul), hatua ya kwanza itahusisha vijana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 12 (wanafunzi wa darasa la tano na la sita wa shule za msingi) na kuwafanya waungane na menzao wa umri tofauti kama ilivyo pangwa.

Kiongozi wa idara ya watoto na makuzi ustadh Sarmad Saalim amesema kua: “Ratiba ya (Rabiu Maarifa ya pili) inayo anza kipindi cha likizo, ni ratiba ya kimalezi inayo saidia kujenga heshima ya mwanafunzi na maadili mema ya kiislamu na kibinadamu na kuandaa kizazi cha watu wanaojitambua wenye uwelewa wa mambo ya dini, pamoja na kuelekeza uwezo wa kiakili na kivitendo katika njia sahihi na kutambua vipaji na kuvilea katika mwenendo sahihi hususan kwa tabaka la vijana ambalo ndia msingi wa jamii”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika ratiba hii ambayo wanashiriki zaidi ya wanafunzi 200 inafanywa baada ya kukubaliana na viongozi wa shule pamoja na ofisi ya malezi ya mkoa wa Karbala na wasimamizi wa mambo ya wanafunzi, ratiba hii inahusisha mambo kadhaa yanayo kuza uwezo wa kiakili na kitamaduni na kukuza vipaji vya kiakili, kuna mambo mbalimbali yanayo endana na umri wa walengwa, ikiwa ni pamoja na:

  • - Hema za Skaut.
  • - Michezo mbalimbali.
  • - Vitendo vya kukomaza akili na mwili.
  • - Safari za kielimu na mapumziko.
  • - Warsha za kielimu na kitamaduni.

Akabainisha kua: “Washiriki wa ratiba hii wamegawika makundi mawili, kundi la kwanza wapo katika jengo la Kuleini lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu na lingine lipo katika Mutanazah Imamu Hussein (a.s)”

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu husimamia na huendesha ratiba mbalimbali za kielimu na kitamaduni zinazo endeshwa mdani na nje ya Ataba tukufu, zinazo lenga kumtumikia mwanafunzi na kumjenga katika dini na tamaduni kwa mujibu wa mwenendo wa Ahlulbait (a.s), sambamba na kujenda moyo wa uzalendo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: