Maahadi ya Imamu Hussein (a.s) ya mihadhara ya wanawake yaanza mwaka mpya wa masomo na yafanya mitihani ya mwezi wa kwanza…

Maoni katika picha
Maahadi ya Imamu Hussein (a.s) ya mihadhara ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu –ambayo inatumia haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi kama makao makuu yake- imefungua mwaka mpya wa masomo kwa hatua tatu (Tamhidi, hatua ya kwanza na ya pili) ikiwa na wanafunzi 168, wameanza masomo tangu mwezi uliopita na sasa hivi wanafanya mitihani ya mwezi wa kwanza katika mwaka huu wa masomo chini ya utaratibu uliopangwa.

Mwaka huu Maahadi imepata mwitikio mkubwa tofauti na miaka iliyo pita, hii ni dalili ya kufanya vizuri kwa wahitimu wake katika sekta ya kutoa mihadhara pamoja na maendeleo mazuri ya wale ambao bado wanaendelea na masomo, Maahadi imeandaa mazingira mazuri ya utoaji wa mihadhara kwa wanafunzi katika majaalis mbalimbali za wanawake, jambo ambalo linasaidia kuonyesha kwa vitendo mambo wanayo soma katika nadhariyya pamoja na kuchukua mazingatio kwa kila mwanafunzi.

Maahadi haijaishia kutoa elimu kwa wanafunzi walio sajiliwa peke yao, bali inajali na makundi mengine ya watu ambao hawana nafasi ya kukaa darasani kwa muda mrefu, wamepangiwa muda maalum kwa ajili ya kunufaika na masomo haya, fahamu kua selibasi ya masomo inayo tumiwa na Maahadi inafanana na selibasi zanazo tumiwa na taasisi zingine za kielimu, masomo yanayo someshwa ni:

  • 1- Qur’an tukufu kwa kufundisha kisomo sahihi.
  • 2-
  • 3-
  • 4-
  • 5- Tafsiri ya Qur’an.
  • 6- Mbinu za utafiti.
  • 7- Uwasilishaji na utoaji wa khutuba.
  • 8-
  • 9-
  • 10- Maendeleo ya binadamu.

Pamoja na mazoezi ya kutoa mihadhara, muda wa masomo ni miaka mitatu, baada ya hapo wanafunzi hutunukiwa vyeti na Maahadi.

Kumbuka kua lengo la kuanzishwa kwa Maahadi hii, ni kuboresha tablighi katika seka ya wanawake kutokana na umuhimu wao hususan katika kipindi cha maombolezo, na kuhakikisha tunawatoa katika uwanja mdogo na kuwaweka katika uwanja mkubwa utakao wawezesha kuelezea tukio la Husseiniyya kwa njia za kisasa na za wazi zinazo eleweka zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: