Maoni katika picha
Hema hizi zinatofautiana na hema zilizo wahi kuwekwa siku za nyuma, namna zilivyo andaliwa na zilivyo fungwa, zimefungwa katika jangwa la Karbala, sehemu ya Kasara ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu karibu na uwanja wa kijani.
Kiongozi wa idara ya uhusiano na vyuo vikuu Ustadh Azhar Rikabi ameongea kuhusu malengo ya hema hizi kua: “Hema hizi zina matokeo mazuri na zimefikia malengo yake, uongozi mkuu wa Atabatu Abasiyya una unga mkono mradi huu, ambao ni sehemu ya harakati za idara ya mahusiano na vyuo vikuu katika mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, ambapo hufanywa kipindi cha likizo kwa ajili ya kunufaika na kipindi hicho”.
Akabainisha kua: “Katika mahema kuna ratiba mbalimbali, kwenye sekta ya dini kuna mihadhara ya Fiqhi na Aqida, pamoja na shindano la kidini, ambapo yaliulizwa maswali ya kidini na kitamaduni, yakiwepo maswali ya Fiqhi, Agida, Sayansi, Historia, Jografia na maswali ya kilugha pamoja na masomo ya utoaji wa mihadhara na maendeleo ya binadamu, pia kulikua na halaqa (vikao) vya majadiliano kuhusu hali ya taifa pamoja na mida ya mapumziko”.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu husimamia na kuendesha ratiba mbalimbali za kielimu na kitamaduni ndani na nje ya Ataba tukufu, zinazo saidia kujenga maendeleo ya wanafunzi na kuimarisha misingi ya dini kwa mujibu wa mwenendo wa Mtume na watu wa nyumbani kwake watakasifu (a.s) pamoja na kujenga maelewano na uzalendo wa taifa.