Maoni katika picha
Hayo yalisemwa katika ujumbe ulio wasilishwa kwa niaba yao na mwanafunzi Abdul-Khaliq Hussein kutoka chuo kikuu cha Bagdad katika hafla ya kukamilisha ratiba ya hema iliyo fanyika katika jangwa la Karbala sehemu ya Kasarah inayo milikiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu karibu na uwanja wa kijani, ambapo alisema kua: “Sisi wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iraq tunatangaza kua hakika leo ni siku ya ushindi na tupo katika hema za fatwa ya ushindi, ni ushindi wa matamanio ulio patikana kutokana na msimamo wa kutekeleza sheria na kupambika na subira na kujitolea na kufanya kazi kama tim moja kwa ajili ya kujenga kizazi chenye mshikamano kitakacho itumikia Iraq na wairaq”.
Akabainisha kua: “Hakika hema hizi zimetuleta pamoja watu wa aina tofauti, waumini wa dini zaidi ya moja, kwa pamoja tumefurahishwa na jambo hili, tumeishi kwa mapenzi makubwa kama ndugu tunao unganishwa na taifa hili, na kukutana katika eneo hili takatifu, ardhi ya Hussein chini ya bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kuanzia hapa tuondoke kwenda kujenga taifa letu upya kama walivyo ondoka wapiganaji watukufu kwenda kukomboa nchi”.
Hali kadhalika katika hafla hiyo, uliwasilishwa ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu na Shekh Kamali Karbalai, kutoka katika kitengo cha dini, ambaye aliwashukuru sana waandaaji na wasimamizi wa mradi huu pamoja na washiriki, alisema kua: “Yapasa mfahamu kua nyie ndio nguzo muhimu ya umma huu, mnatakiwa kuyashinda mazingira tunayo pitia kama umma na kupambana na changamoto zote pamoja na vitimbi vya matwaghuti, tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliye tuwezesha kulinda misingi ya utukufu wetu na taifa letu”.
Akaongeza kua: “Mnaweza kuhisi jambo hili na kujikumbusha namna gani tulivyo pata ushindi kama taifa la Iraq, ni kupitia damu tukufu za wairaq, walipo jitokeza kuitikia wito wa Marjaa dini mkuu wa kuihami Iraq na maeneo matakatifu na kuhifadhi utukufu wa taifa hili kwa kukiamgamiza kikundi cha shetani”.
Karbalai akawaambia wanafunzi kua: “Nyie ndio nguvu inayo tegemewa katika siku za usoni, asighafirike yeyote kuhusu nguvu yake, nyie ndio watoa maamuzi na nyie ndio tofali zinazo jenga jamii hii taifa linakutegemeeni sana”.
Pia kulikua na mambo mengine yaliyo fanyika katika hafla hiyo ikiwa ni pamoja na uimbaji wa qaswida za kimashairi, igizo hukusu mashahidi wa Iraq kisha zikatolewa zawadi kwa walio fanya vizuri katika program za hema.
Program hii ilihitimishwa ndani ya malalo ya Abufadhil Abbasi (a.s) kwa kugawa vyeti kwa washiriki wote wa ratiba za hema, huku wakiomba kuendelea program hii siku za mbele.
Kumbuka kua shuguli hii imeandaliwa na kusimamiwa na idara ya mahusiano na vyuo vikuu chini ya kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ikiwa ni sehemu ya mradi wa kijana wa Alkafeel mzalendo, kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iraq na wameshiriki zaidi wa wanafunzi (150), kutoka katika vyuo vikuu (25) program imeitwa (Hema za fatwa ya ushindi) kufuatia ushindi uliopatikana kupitia jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi kwa kukomboa ardhi yote ya Iraq kutoka mikononi mwa magaidi ya Daesh, hema hizi zilikua tofauti na hema za Skaut zilizo wahi kuwekwa siku za nyuma, kutokana na mpangilio wake, hema hizi zimefungwa katika jangwa la Karbala eneo la Kasarah lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu karibu na uwanja wa kijani.