Ratiba ya kufunga program hii imefanyika katika bustani za Jumuiya ya Skaut, na kulikua na mambo mbalimbali, yanayo saidia kufikia lengo kuu; ambalo ni kuwajenga kiakili na kiutamaduni na kuendeleza vipaji vyao vya kiakili na kimwili, hivyo kulikua na mambo yanayo endana na rika zao, miongoni mwa mambo hayo ni, kufunga hema za Skaut, mashindano mbalimbali, mafundisho ya kielimu pamoja na safari za mapumziko na vitu vidogo vidogo vya kuongeza uwezo wa akili.
Maandalizi yanaendelea ya kufanya program nyingine ya Skaut kwa kikundi cha wanafunzi wenye umri wa miaka 13 hadi 15 na kundi lingine la umri wa miaka 15 hadi 18, kila kundi litakua na mambo yake tofauti na lingine kutokana na kutofautiana umri wao, kwa jina hilo hilo la (Rabiu Maarifa awamu ya pili), mambo yatakayo fanyika ni:
- - Kutakua na mihadhara ya kidini na ki-akhlaq.
- - Safari za mapumziko.
- -
- -
- - Vitu vingine vidogo vidogo.
Mambo yatakayo kuwepo katika kikundi cha pili cha Skaut ni kama yafuatayo:
- - kutakua na mihadhara ya Fiqhi na Aqida.
- - Kutakua na mihadhara elekezi.
- - Kutakua na mihadhara kuhusu maendeleo ya mwanadamu.
- - Masomo ya kielimu na kitamaduni yenye mada mbalimbali.
- - Kutakua na mihadhara kuhusu utoaji wa huduma ya kwanza.
- - Kutakua na mashindano pamoja na ratiba ya mabumziko.
- - Kutakua na safari za kutembelea Ataba tukufu za Karbala na maeneo mengine ya kihistoria.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu huandaa na kusimamia program nyingi za kielimu na kitamaduni, ndani na nje ya Ataba tukufu, zinazo lenga kujenga misingi imara ya dini tukufu ya kiislamu na kutoa mafundisho kwa mujibu wa mwenendo wa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) pamoja na kujenga uzalendo wa taifa.