Maoni katika picha
Ratiba yenyewe ni hema la kitamaduni lililo kua na mambo mbalimbali yanayo endana na kiwango cha elimu na umri wa washiriki, chini ya usimamizi wa kamati ya watalam walio bobea, na kulikua na mihadhara elekezi ya kidini na kuhusu maendeleo ya kibinadamu, pamoja na vipindi vya mapumziko na kutembelea Ataba tukufu na miradi ya Atabatu Abbasiyya ya kiviwanda na kielimu.
Wakati wa kufunga ratiba ya hema washiriki wote walipewa vyeti vya ushiriki, na wale walio fanya vizuri katika mashindano wakapewa zawadi.
Fahamu kua ratiba hii iliandaliwa kwa ajili ya kunufaika na kipindi cha likizo na kuongeza elimu na maarifa pamoja na kulea vipaji na kuwafanya waweze kutumia vipawa vyao katika maisha ya nyumbani na chuo, hali kadhalika kuwaweka karibu na malalo ya maimamu wao, ambayo ni moja ya vituo muhimu kielimu na kiutamaduni kutokana na harakati mablimbali zinazo fanywa na malalo hizo tena katika sekta tofauti.