Maoni katika picha
Katika Alkhamisi hii ambayo imesadifu kipindi cha likizo, idadi ya mazuwaru imeongezeka mara dufu, pia kutokana na hali ya hewa kua nzuri inayo muwezesha mtu kuja na familia yake kufanya ziara katika Ataba hizi bila ugumu wowote.
Mahudhurio matukufu haya sio ya raia wa Iraq peke yake, bali kuna idadi kubwa ya mazuwaru wanaotoka katika nchi za kiarabu na kiislamu, watumishi wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) wanafanya kila wawezalo kuwarahisishia mazuwaru watukufu waweze kufanya ziara na ibada zao kwa amani na utulivu, pia mawakibu (vikundi) vya kutoa huduma vimeenea kila kona katika maeneo yanayo zunguka haram mbili tukufu kwa ajuli ya kuwahudumia mazuwaru watukufu.
Kumbuka kua kuna riwaya nyingi zinazo sisitiza umuhimu wa kumzuru Imamu Hussein (a.s), miongoni mwa riwaya hizo ni: Kutoka kwa Abdillahi Twahani, kutoka kwa Abu Abdillahi Swadiq (a.s) anasema: nilimsikia akisema: (Hakuna mtu yeyote siku ya kiyama ispokua atatamani kua miongoni mwa mazuwaru wa Hussein, kwa yale atakayo ona wakifanyiwa mazuwaru wa Hussein (a.s) kutokana na utukufu wao mbele ya Mwenyezi Mungu s.w.t).