Leo ni siku ya huzuni kwa wafuasi na wapenzi wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) ni siku ya kufariki kwa bwana wa karama Qassim mtoto wa Imamu Mussa Kaadhim (a.s) ambaye alifariki mwezi ishirini na mbili Jamadal-Awwal mwaka wa (192h).
Imamu Qassim (a.s) alisafiri kutoka katika mji wa babu yake Mtume (s.a.w.w) kuelekea Iraq akiwa katika msafara wa wafanya biashara kwa ajili ya kujificha asijulikane na maadui waliokua wakimtesa baba yake Imamu Kaadhim (a.s), kutokana na nafasi yake ya kuendeleza familia ya Mtume ambayo ni chemchem ya hekima na elimu na nafasi yao ya ubaba na huruma kwa waumini. Alawiyyiina walipata pateso na manyanyaso mbalimbali jambo lililo pelekea watoto wa Imamu Mussa Kaadhim (a.s) kusambaa sehemu mbalimbali za dunia kwa ajili ya kujaribu kulinda heshima ya Imamu Ridha (a.s) pamoja na Qassim (a.s) aliye julikana kwa ukubwa wa elimu yake na ukomavu wa akili yake.
Alikua (a.s) mwenye heshima kubwa, mtakasifu anatokana na kizazi cha Mtume na alirithi utukufu kutoka kwa Maimamu (a.s), pia ni mtu wa pekee aliye pata mitihani na matatizo mengi katika zama zake baada ya kaka yake Imamu Ridha (a.s), yatosha kuelezea utukufu wake kwa kunukuu riwaya iliyo pokelewa na Thiqatul-Islaam Shekh Kuleini katika kitabu cha Al-Kaafi isemayo: Kutoka kwa Imamu Mussa Ridha (a.s) kutoka kwa Yazidi bun Saliit kutoka kwa Imamu Kaadhim (a.s) wakiwa katika njia ya kueliekea Maka Imamu Alimuambia: (…Nakuambia ewe baba Ammaarah mimi nilipo toka nyumbani nilimuhusia mwanangu fulani, nikamshirikisha na wanangu wengine kwa Dhahiri na nikamuhusia kwa siri, nikamtenga peke yake, lau kama jambo hili (uimamu) lingekua kwa matashi yangu ningempa mwanangu Qassim kwa namna ninavyo mpenda na kumuamini, lakini jambo hili lipo chini ya maamuzi ya mwenyezi Mungu mtukufu humpa amtakaye).
Qassim (a.s) alifariki baada ya kuugua sana mwaka wa (192h) katika ardhi ya Suri mtaa wa Bakhamra, sehemu ambapo kaburi lake na kubba lake lipo hadi sasa, likiwa linang’aa dhahabu na kutoa nuru ya utukufu kutokana na karama zake zilizo shuhudiwa na watu wa karibu na wa mbali, akasifiwa na kila mwenye kusifu na watu wakamhifadhi katika mimbari ya fahari sana iliyopo ndani ya nyoyo zao.
Miongoni mwa wasia wake (a.s) kwa Ammi yake Shekh Hayyi ambaye alioa mmoja wa mabinti zake, alimuusia kua: (Ewe Ammi! Nitakapo kufa unioshe, univishe sanda na kunizika, msimu wa hijja ukifika nenda kahiji pamoja na huyu binti yangu, ukimaliza ibada ya hijja, nenda Madina pamoja naye, mkifika katika mlango wa Madina muache atamgulie wewe na mke wangu mtembee nyuma yake, ataenda kugonga mlango katika nyumba tupu, hiyo ndio nyumba yetu, ataingia katika nyumba hiyo na atawakuta wanawake wajane).
Mwaka wa pili baada ya kufariki kwa Qassim (a.s), Shekh Hayyi alikwenda hijja akafuatana na binti wa Qassim (a.s), ikawa kama alivyo sema Qassim (a.s), binti huyo alikwenda kugonga mlango akafunguliwa, akazungukwa na wanawake wa bani Hashim, wakaanza kumuuliza jina lake na jina la baba yake, mama yake Qassim alipo muona tu akaanza kulia huku akisema: (Waa waladaahu waa Qaassimaahu… Wallahi huyu ni yatima wa Qassim), kisha binti akawaambia kua babu yake na mama yake wamesimama mlangoni, inasemekana kua mama yake Qassim aliugua baada ya kusikia kifo cha mwanae Qassim, akaishi siku tatu kisha akafa.
Shekh Kuleini pia amepokea riwaya kutoka kwa Suleiman Jafari ya kwamba alisema: Nilimuona Abu Hassan (a.s) wakati alipo karibia kufariki mmoja wa watoto wake alimuambia mwanae Qassim: (Simama ewe mwanangu umsomee ndugu yako (waswafaat swaffaa) mpaka uimalize, akasoma alipo fika katika aya isemayo (… Ahum ashaddu khalqan am man khalaqnaa…) ndugu yake akafariki, katika riwaya hizi mbili zinaonyesha namna Imamu alivyo kua akimjali zaidi mwanae Qassim (a.s).
Katika utukufu wa ziara yake (a.s), Sayyid ibun Twausi katika kitabu chake cha Misbaahu Zaairiina, amefuatanisha ziara ya Qassim mtoto wa Imamu Kaadhim (a.s) na ziara ya Abulfadhil Abbasi mtoto wa kiongozi wa waumini na Ali Akbar mtoto wa Imamu Hussein (a.s), alipo sema: (Ziara za waja wema watoto wa maimamu (a.s) ukitaka kumzuru mmoja wao kama vile Qassim bun Kaadhim na Abbasi bun Amirulmu-uminina au Ali bun Hussein aliye uliwa Karbala, na walio katika nafasi yao.
Kuna hadithi imepokewa kutoka kwa Imamu Ridha (a.s) kua alisema: (Atakaye shindwa kuja kunizuru mimi basi amzuru ndugu yangu Qassim).