Chini ya wakufunzi bora hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu, mradi wa kitaifa wa kuandaa wasomaji umeingia hatua yake ya tatu…

Maoni katika picha
Mkuu wa kituo cha miradi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya ametangaza kuanza kwa hatua ya tatu ya mradi wa kitaifa wa kuandaa wasomaji hapa Iraq, akasisitiza kua hatua hii itakua ya aina yake na itakamilisha mazuri yaliyo kuwepo katika hatua mbili za kwanza.

Sayyid Hussein Halo akaongeza kusema kua: “Kutakua na semina mbili zitakazo simamiwa moja kwa moja na wakufunzi mahiri kwa viwango vya Iraq na ulimwengu wa kiislamu, ambao ni: (Ustadh Sayyid Mahdi Sefu, Ustadh Ahmad Abu Qassim, Ustadh Sayyid Abbasi Anjaam kutoka Iran, na Dokta Raafii Aamiri, Ustadh Shekh Maitham Tammaar, Ustadh Sayyid Hussein Halo na Ustadh Ali Bayati kutoka Iraq), kila Ustadh atasimamia kile alicho bobea kuanzia Tajwid, waqfu, Ibti-daai, Sauti na Nagham”.

Akabainisha kua: “Hali kadhalika watafundishwa masomo kuhusu Qur’an tukufu na Mheshimiwa Sayyid Alaa Hasani”.

Akaashiria kua: “Hakika usomaji wa washiriki wa semina, wao ndio mustaqbali wa Iraq, wakiweza kutumia vizuri fursa hizi, ambazo wanakutana na walimu wenye kiwango cha juu, jambo hili litasaidia kuinua kiwango cha Qur’an hapa Iraq na hatimae kua na wasomi bora zaidi”.

Mkuu wa kituo cha kitaifa cha maarifa ya Qur’an katika wakfu Shia Dokta Raafii Aamiri amesema katika ujumbe alio toa wakati wa ufunguzi kua: “Kuna umuhimu mkubwa wa wasomaji wanaoshiriki katika semina hii wanufaike na uzowefu mkubwa kutoka kwa wakufunzi wa semina, na wafanyie kazi yale watakayo fundishwa katika usomaji wao, hususan wao wapo katika nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa, pia napongeza juhudi zinazo fanywa na kituo cha miradi ya Qur’an katika Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya”.

Kumbuka kua mradi wa kitaifa wa kuandaa wasomaji wa Qur’an hapa Iraq ni moja ya miradi iliyo anzishwa na kituo cha miradi ya Qur’an cha Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya tangu mwaka (2013) unalenga kuandaa wasomi bora wa Qur’an tukufu na fani zake, hii ni program kamili ambayo ina vipengele vingi vilivyo pasishwa na wasomi wakubwa kutoka Misri na wakapata shahada ya kutambuliwa na ubora.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: