Maoni katika picha
Hema hizi wanashiriki wanafunzi (85), kutakua na mambo mbalimbali kama vile; mihadhara kuhusu maendeleo ya wanadam, na maendeleo ya taifa, mashindano ya Qur’an, mazoezi ya asubuhi, vipindi vya mapumziko na kutakua na mambo ya kitamaduni pamoja na maelekezo ya namna ya kutoa huduma ya kwanza ya uokozi, na kutembelea maeneo ya makumbusho.
Ustadh Azhar Rikabi ambaye ni kiongozi wa idara ya mahusiano na vyuo vikuu ametuambia kuhusu hema hizi kua: “Upekee ya hema hizi ni kwamba zipo mbali na mji wa Karbala, zimefungwa katika eneo ya Kasarah linalo milikiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika jangwa la Karbala karibu na uwanja wa kijani”.
Akaongeza kusema kua: “Mazingira ya hali ya hewa imekua changampto kwa washiriki, kwa sababu ni mara ya kwanza wanaishi katika mazingira ya aina hii, watakaa na kulala ndani ya hema, ambazo zimewekwa kwa makundi, kila hema litakua na kiongozi kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma na utekelezaji wa ratiba”.
Atabatu Abbasiyya tukufu imeanzisha mradi huu kwa ajili ya kujenga mazingira ya kuimarisha umoja na uzalendo, vitu walivyo navyo wanajeshi wetu watukufu walio linda ardhi ya taifa hili, Ustadh Rikabi akaongeza kusema kua: “Kuna baadhi ya mafundisho na maelekezo ambayo yanatolewa kwa washiriki yanawajenga katika kujitegemea, kumbuka hizi ni hema za Skaut, tunatoa mafunzo elekezi ya kujitegemea na namna ya kuleta maendelea hili ndio lengo kubwa la hema hizi”.
Mwisho wa mazungumzo yake akafafanua kua: “Hakika ratiba ya program za hema inastarehesha sana pamoja na kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo, kuna kundi maalumu katika mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel chini ya idara ya mahusiano na vyuo vikuu watakao fanya kazi ya kuwahudumia washiriki”.