Kwa bei nafuu na huduma bora: Idara ya kunufaika na mitambo ya Atabatu Abbasiyya yatangaza ratiba ya safari za kutenbelea Ataba za Iraq…

Maoni katika picha
Idara ya kunufaika na mitambo ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza ratiba za safari za kutembelea Ataba na mazaru tukufu ya Iraq katika mwaka huu, kwa bei nafuu na huduma bora tena kwa kutumia magari ya kisasa. Kwa mujibu wa maelezo ya idara hiyo ratiba ya safari imegawanywa katika siku za wiki kama ifuatavyo:

Juma Pili: Kutembelea watoto wa Muslim bun Aqiil (a.s) pamoja na kutembelea Atabatu Kadhimiyya tukufu. Nauli ya mtu mmoja ni (dinari 5000), safari itaanza saa moja asubuhi katika mlango wa Bagdad – karibu na Screen.

Juma Nne: Kutembelea Atabatu Alawiyya tukufu na Masjid Kufa pamoja na maeneo yanayo fungamana na Masjid hiyo, ikiwa ni pamoja na Masjid Sahla. Nauli ya mtu mmoja ni (dinari 4000), safari itaanza saa saba mchana katika mlango wa Bagdad – karibu na Screen.

Ijumaa: Kutembelea Atabatu Askariyya tukufu na malalo ya Sayyid Muhammad (a.s). Nauli ya mtu mmoja ni (dinari 9000) safari itaanza saa kumi na mbili asubuhi katika mlango wa Bagdad – karibu na Screen.

Idara imesisitiza kua nafasi zipo, na safari ni kwenda na kurudi, kwa kukata tiketi au kupata maelezo zaidi unaweza kutembelea ofisi zetu zifuatazo:

Ofisi ya kwanza: Ipo karibu na mlango wa Bagdad katika jengo la Imamu Askariy (a.s), zamani likijulikana kama (Hoteli ya Dalla).

Ofisi ya pili: Ipo karibu na stendi ya Saaqi katika barabara ya Maitham Tammaar – mkabala na hospitali ya Maitham Tammaar.

Au piga simu kwa namba zifuatazo: 07602326779 / 07602327074 / 07801952463.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: