Kwa tafiti kumi na tano za kielimu limechapishwa jarida la tano miongoni mwa majarida ya kielimu…

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha (Ameed duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaat) chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa jarida la tano ambalo ni namba (tisa na kumi) miongoni mwa majarida yaliyo jaa elimu, lenye namba ya kimataifa (ISSN) na namba yake ya usajili katika mtandao ni (5721-2312).

Jarida la tano limebeba tafiti nyingi (zinafika kumi na tano) miongoni mwa tafiti boro za kielimu, tafiti saba zimeandikwa kwa lugha ya kiarabu huku tafiti nane zikiandikwa kwa kiengereza, miongoni mwa tafiti hizo ni: (Fizikia, kemia, sayansi ya viumbe hai, hesabu, uhandisi na kompyuta..).

Kwa mujibu wa maelezo ya kamati mbili (ya ushauri na ya wahariri) wa jarida hili: “Hakika idadi mpya ya jarida hili imejaa elimu kubwa, kuna masomo ya mambo ya mazingira na masomo ya uhandisi, tuna tarajia litaziba mwanya wa elimu inayo hitajiwa na watafiti, na litathibitisha uhakika wa elimu inayo hitajika na watafiti, na tumezingatia mnyambuliko wa mada kutokana na aina za ubobezi kwa ajili ya kutekeleza matakwa ya wasomaji na wafuatiliaji wa jarida hili, ambalo leo hii -kutokana na juhudi za wasimamizi na wahariri wake- limefanya vizuri katika kufikia matarajio ya watafiti, hususan sekta ya usambazaji imefanya vizuri kulifikisha katika nafasi ya majarida ya kimataifa”.

Kumbuka jarida hili, lilianzishwa kwa malengo maalum, miongoni mwa malengo hayo ni kuimarisha mawasiliano baina ya watafiti wa kiiraq na walio bobea kutoka katika vyuo mbalimbali vya Iraq, na kutoa nafasi ya kuongeza elimu, na kutengeneza kundi la watalam watakao fanya kazi bega kwa bega katika mambo ya kielimu yenye msingi, pamoja na kujielekeza katika utafiti kama kikundi (jopo) na kutoa nafuu kwa mtafiti mmoja mmoja, na kulifanya jarida hili kua tegemezi kimataifa kutokana na kiwango cha elimu inayo patikana ndani yake, elimu ya mazingira na uhandisi, na kusaidia kutia hamasa na changamoto kwa wasomi wa kisekula wanaofanya ubobezi, kupitia jarida hili pia tunaweza kusambaza tafiti bora za kielimu.

Ukitaka kuwasiliana na wahusika wa jarida au kushiriki, unakaribishwa kutembelea mtandao ufuatao: https://albahir.alkafeel.net/
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: