Shindano hilo litafanyika sambamba na kongamano litakalo endeshwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu linalo adhimishwa kila mwaka kufuatia kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda, litakalo fanyika chuni ya kauli mbiu isemayo (Ushindi umetokana na nyie ni wenu na nyie ndio wenye nao) kuanzia mwezi 13 – 14 Shawwal 1439h, sawa na 28 – 29 Juni 2018m.
Kamati imeweka masharti yafuatayo ya kujiunga na shindano hili:
- 1- Mshiriki ana haki ya kuchagua aina ya uandishi atakao ona unafaa (makala ya rai, Makala ya utunzi au Makala ya simulizi) cha msingi ihusu fatwa tukufu ya kujilinda au Hashdi Sha’abi.
- 2- Makala ihusu ushujaa wa Hashdi Sha’abi kwa ujumla (na sio mtu maalum) katika kulinda kwao taifa misingi ya ubinadamu na utunzaji wa mazingira.
- 3- Makala iandikwe kwa lugha faswaha ya kiarabu, na iwe na sifa za Makala –muonekano mzuri, lugha sahihi, uwiyano wa vifungu vyake na ufupisho-.
- 4- Isiwe imesha wahi kutolewa siku za nyuma, na iwe ya mshiriki mwenyewe sio ya kunakili kutoka sehemu nyingine au aliyo andikiwa na mtu mwingine.
- 5- Isiwe na maneno chini ya (300) na yasizidi (700).
- 6- Isiashirie ubaguzi na matusi au vitu vinavyo fanana na hayo, jambo ambalo ni kinyume na maadili mema.
- 7- Hairuhusiwi kwa mshiriki kuandika Makala zaidi ya moja.
- 8- Kamati ya maandalizi inahaki ya kuondoa kwenye shindano Makala yeyote ambayo haitatimiza masharti yaliyo tajwa.
- 9- Zawadi inaweza kuzuiwa iwapo kamati ya maandalizi itajiridhisha kutokuwepo kwa uwiyano wa kazi iliyo wasilishwa na ushindi.
- 10- Hairuhusiwi kwa mshiriki kuomba Makala yake baada ya kuikabidhi, itabaki chini ya usimamizi wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu.
- 11- Makala iandikwe kupitia program ya (ward) na ihifadhiwe kwenye (CD) ikiwa pamoja na wasifu (cv) ya muandishi, pia unaweza kutuma kupitia barua pepe ifuatayo (info@holyfatwa.com)
- 12- Mwisho wa kupokea Makala za kushiriki ni (21 Juni 2018m).
- 13- Makala tano za kwanza zitazawadiwa kiasi cha (100,000) dinari laki moja za Iraq.