Kamati inayo simamia shindano hili imeweka masharti yafuatayo:
- A- Kisa kiandikwe kwa kufuata misingi ya kiutalamu na maadili ya watoto.
- B- Kielezee ujasiri wa jeshi la Iraq na Hashdi Sha’abi kwa ujumla (sio kumuelezea mtu maalum) katika kulinda taifa na misingi ya ubinadamu na jinsi walivyo linda mazingira na maeneo matakatifu.
- C- Kisa kisiwe kimesha wahi kuandikwa katika kitabu au mitandaoni au kimesha wahi kutolewa katika shindano lingine.
- D- Kiandikwe kwa kutumia program ya (ward) na kihifadhiwe kwene (CD) kisha kikabidhiwe kwenye kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kikiwa pamoja na wasifu (cv) ya muandishi, au kinaweza kutumwa kwenye mtandao wa kimataifa Alkafeel ambao ni (alkafeel.net) au kwenye anuani ifuatayo (info@holyfatwa.com).
- E- Mwisho wa kupakea ni tarehe 21 Juni 2018m.
- F- Zimeandaliwa zawadi kwa visa vitano vitakavyo faulu ambazo ni (200,000) dinari laki mbili za Iraq.