Wanachuoni wa dini na watafiti wa kiiran waipongeza Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuhifadhi turathi na waisifu kua ni ya kipekee…

Maoni katika picha
Jopo la maulamaa wa dini na watafiti wa mambo ya turathi katika Jamhuri ya kiislam ya Iran, wamesifu kazi inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, katika sekta ya kuhifadhi na kuzienzi turathi za kiislam, na kuzitangaza kwa utaratibu mzuri baada ya kuzihakiki na kuzichapisha, wamesema kua hilo ni jambo zuri na lina matunda mazuri.

Hayo yamesemwa katika vikao vinavyo fanywa na ujumbe wa kitengo cha maarifa ya kiislam na kibinadam cha Atabatu Abbasiyya tukufu unao ongozwa na rais wa kitengo hicho Shekh Ammaar Hilali, pamoja na wanachuoni wa dini na wahakiki katika jamhuri ya kiislam ya Iran, vikao hivyo vinafanyika kwa lengo la kujenga ushirikiano, na kutambulisha mafanikio ya Ataba tukufu katika sekta hii.

Mheshimiwa Sayyid Jawaad Shaharistani mwakilishi wa Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Sistani amebainisha kua: “Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu wanastahiki pongezi kwa juhudi kubwa ya kutunza athari za wanachuoni wetu wakubwa, hakika taasisi ya Aalul-Bait (a.s) ya turathi ambayo ipo chini ya ofisi ya Marjaa dini mkuu pamoja na taasisi zingine zilizo chini yake ambazo zinafika taasisi thelathini, zoto kwa ujumla ziko tayali kuihudumia Atabatu Abbasiyya tukufu na milango yake iko wazi kwa ajili ya kufanya kazi kwa ushirikiano”.

Naye Mheshimiwa Ayatullahi Shekh Lutfillah Swafi amesema kua: “Hakika harakazi za kielimu na kitamaduni zinapata maendeleo makubwa katika nchi ya Iraq kwa ujumla na hasa katika Ataba mbili kutokana na juhudi zenu tukufu, hii ni fursa nzuri yapasa kuitumia na kuonyesha turathi za kiislamu na kuzitangaza zaidi”.

Mheshimiwa Sayyid Alawi Burujurdi amesifu mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu na akasema kua yuko tayali kubadilishana nao nakala za maandishi na picha, maktaba ya Sayyid Burujurdi ina zaidi ya nakala (150,000) laki moja na eflu hamsini zenye maudhui mbalimbali, akasisitiza umuhimu wa kuhakiki nakala kwani kwa kufanya hivyo zitahifadhika na hatutapoteza turathi tetu adhim za kiislam.

Baada ya matembezi ya kielimu yaliyo fanywa na ujumbe wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika taasisi ya nakala kale, inayo fanya kazi ya kutunza nakala kale na kuziwekea faharasi, pamoja na kufahamu miradi yake ya baadae, miongoni mwa miradi hiyo ni kurahisisha utafutaji wa faharasi za nakala kale duniani, Sayyid Mujtaba Mujani amesisitiza kua taasisi ya nakala kale ipo tayali kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta zote.

Kumbuka kua ziara hii inalenga kufungua milango ya kusaidiana na kufanya kazi pamoja, na kuangalia utendaji wa taasisi zilizo tembelewa na ugeni huo, jambo ambalo faida yake inarudi kwa wote, na kwa upande mwingine ilikua ni fursa ya kuelezea harakati zinazo fanywa na kitengo hiki katika sekta zote zinazo husiana nacho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: