Kukamilika kwa program ya hema za Skaut (Fatwa ya ushindi) awamu ya pili kwa wanafunzi wa sekondari…

Maoni katika picha
Wanafunzi wa sekondari wanao shiriki katika hema za Skaut za fatwa ya ushindi awamu ya pili wameomba kurudiwa program hii zaidi ya mara moja ndani ya mwaka, kwani wamenufaika sana na wameweza kutumia kipindi cha likizo kwa manufaa na muelekea sahihi.

Hema za fatwa ya ushindi zinazo simamiwa na idara ya mahusiano na vyuo vikuu chini ya kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel umekuja kama sehemu ya kukamilisha program ya hema iliyo tangulia kufanywa kwa wanafunzi wa vyuo, katika hema hizi wameshiriki zaidi ya wanafunzi 85 kutoka katika mikoa mitano, ambayo ni: (Karbala, Baabil, Qadisiyya, Muthannah na Dhiqaar), na imedumu siku nne katika eneo la jangwa la Karbala sehemu ya Kasaarah inayo milikiwa na Atabatu Abbasiyya.

Ufungaji wa ratiba ya hema umefanywa siku ya Juma Nne (26 Jamadal-Awwal 1439h) sawa na (13 Februari 2018m) na kuhudhuriwa na ujumbe ulio wakilisha Atabatu Abbasiyya, baada ya kusikiliza Qur’an ya ufunguzi pamoja na mwimbo wa taifa na ule wa Atabatu Abbasiyya, ulifuata ujumbe wa Shekh Daakhil… ambae alibainisha kua: “Watoto wetu watukufu.. lazima kila mmoja wenu ana kisa katika siku hizi chache mlizo ishi hapa, sio vibaya ikiwa kila mmoja ataandika namna alivyo tumia na kunufaika na saa alizo kua hapa, na nini mapendekezo yake ya baadae iwapo akipewa nafasi nyingine.

Yawezekana miongoni mwa faida muhimu ukawa unalinganisha maisha yako ya nyuma na ya sasa, ukamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema aliyo kupa kupitia familia yako na mji wako, na ukamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema aliyo tuneemesha, uzewefu wako unaweza kua katika sekta nyingi, wengi wenu mnatarajia kua na maisha mazuri, miongoni mwa misingi ya kufikia jambo hilo ni mtu kujifundisha kua na subira.

Watoto wetu watukufu.. maisha sio kitu chepesi, haya mliyo yaona ni kidogo sana ukilinganisha na matatizo wanayo pata watu wengi, pengine uzowefu wa matukio ya hivi karibuni waliyo pitia Hashdi Sha’abi na baba zenu, yalikua ni makubwa mno, walikua wanaweza kukaa siku nzima bila kupata maji ya kunywa wala chakula, pengine hawapati hata nusu saa ya kulala, mambo kidogo mliyo pitia waliyaishi baba zenu, marafiki zenu na ndugu zenu”.

Kisha ukafuata ujumbe wa wanafunzi walio shiriki katika ratiba ya hema, ulio wasilishwa kwa niaba yao na mwanafunzi mwenzao Hussein Alaa, ambae alisema kua: “Hakika kazi kubwa imefanywa kwa ajili yetu hadi kukombolewa kwa nchi yetu, tunamuomba Mwenyezi Mungu awalipe kila la kheri, kwa kukesha kwao huku sisi tukiwa katikati ya ndoto, katika siku zile ambazo dakika zake zilitupa hamasa ya kujifundisha mambo mengi tuliyo kua hatuyajui”.

Baada ya hapo ikaimbwa kaswida ya kimashairi iliyo husu kuwapenda watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na kulipenda taifa, hafla ikahitimishwa kwa kupewa vyeti wanafunzi wote walio shiriki katika ratiba ya hema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: