Sayyid Swafi: Fatwa ya Marjaa iliamsha umma na kutufanya tupate ushindi ndani ya miaka mitatu badala ya makadirio ya maadui ya miaka thelathini…

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amebainisha kua: “Marjaa mtukufu alipo toa fatwa kuhusu wale walio leta ufisadi katika ardhi, umma uliamka kutoka usingizini, wakapigana na kundi hilo na wakapata shahada, miongoni mwa mashahidi hao kuna ambao walikua hawaja balehe na wengine ni vikongwe wa miaka zaidi ya themanini, baada ya umma kujiamini walifanikiwa kuwafukaza Daesh, miongoni mwao kuna walio uliwa na wengine wakakimbia ndani ya muda mfupi, nchi ikarudisha heshima yake, makadirio ya baadhi ya nguvu za kiaskari yalikua ni kwamba vita hiyo itadumu kwa miaka (30), lakini vijana wa Iraq wamemaliza vita ndani ya miaka (3), hii ni aibu kwa walio kadiria kua vita itadumu kwa miaka (30), na ni heshima na utukufu kwa wapiganaji wetu walio weza kumaliza vita ndani ya miaka (3), yapasa matukio haya yasipite bure, yatupasa tunufaike nayo na tuyatunze”.

Amesema hayo katika khutuba aliyo toa wakati wa ufunguzi wa nadwa ya kielimu, inayo simamiwa na kituo cha faharasi na kupangilia maalumati kilicho chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abasiyya tukufu.

Akaongeza kusema kua: “Bila shaka elimu imepanuka sana, na mwanadamu wa sasa amenufaika sana katika historia ya wanadamu, elimu hizo zimeandikwa na kutunzwa, leo ulimwengu unabobea katika mambo mbalimbali, na hili ndio tunalo taka, ubobezi huo kwa upande fulani una madhara na kwa upande mwingine una faida, manufaa ni mengi zaidi kuliko madhara, ulimwengu unahitaji wakati mwingi na juhudi kubwa ili kuto zipoteza baadhi ya elimu zinazo weza kusaidia katika ubobezi huo, kawaida ya ubobezi hua ni kufanya mazingatio wakati wa uchambuzi wa fikra fulani, mwanadamu hujitahidi kuonyesha usahihi wa fikra hiyo na kua anaweza kuitunza na kuihami pamoja na kuondoa utata na kuilinda kadri ya uwezo wake”.

Akabainisha kua: “Baadhi za elimu zimemnufaisha sana mwanadamu na kumfikisha katika hatua kubwa zaidi, tukiangalia misingi iliyopo inaonyesha kumlinda mwanadamu asidumbukie kwenye makossa, misingi hiyo ndiyo ambayo anatakiwa kuisimamia mtu anaye fanya utafiti, na siri ya hilo ni kwamba elimu imeenea, lakini bado kuna baadhi za turathi hazija ainishwa, nakusudia turathi za kielimu, hati na namba, watafiti wanao tumia vifaa vya kisasa wanatafuta nakala kale na kuzihakiki pamoja na kuzitambulisha kwa walimwengu”.

Akaendelea kusema kua: “Mitambo yetu ya uchapishaji imeendelea sana, na katika kila nchi kuna idadi kubwa ya machapisho, lakini jambo hili linahitaji utalamu na maarifa, madam faharasi ni miongoni mwa elimu za mitambo, yawapasa watafiti wafanye juhudi ya kuhakikisha elimu hii inakua rahisi kwao, ili mtu asitumie muda mwingi katika utangulizi”.

Akaongeza kusema kua: “Faharasi kwa sasa haina maana ya kutaja majina ya milango kwa wanafunzi, mimi kama msomaji ninapo ingia maktaba inayo tumia namba, namna gani atafanya mtunza maktaba, atanitaka nisome na kuangalia kilichopo ndani ya maktaba, kama hakuniandalia mazingira mazuri ya kusoma jambo hilo litakua doa katika kazi yake, ananitaka nisome lakini hajatengeneza mazingira ua kusoma, faharasi inamrahisishia msomaji kupata anacho kitaka kwa muda mfupi, tuna mshukuru Mwenyezi Mungu kwa kipindi kifupi elimu hii imepata maendeleo makubwa, na Atabatu Abbasiyya ina nafasi kubwa katika kuendeleza elimu hii kama inavyo onekana katika baadhi ya nadwa na makongamano, na hiki ndio kiu cha watafiti, lakini bado nafsi zetu hazijaridhika, hakika elimu hata kama utatoa juhudi zako zote yenyewe haitakupa maarifa yote”.

Sayyid Swafi akatoa wito kwa wasimamizi wa kituo hiki, wajitahidi kufikia viwango vya juu na wanufaike na maendeleo yaliyopo katika sekta ya faharasi na waweke athari katika elimu hii, akawashajihisha wawe na fikra mpya za kiubunifu, kwa lengo la kuhakikisha wanakua na utajo wa kudumu katika sekta hii.

Akaashiria kua: “Hakika yaliyo jiri katika taifa siku za nyuma, na njia ambazo magaidi walitumia kuteka baadhi ya miji ya Iraq, ni njia za kigaidi na kuhofisha, wamefanya utafiti katika hilo na kusomea namna ya kuingiza hofu katika nyoyo za watu, kwa kiwango fulani iliwasaidia hadi baadhi ya watu walikua wanajisalimisha kwao, pamoja na kwamba baadhi ya waliojisalimisha walikua na uwezo wa kupambana nao, lakini walishindwa mbele yao kupitia vita nya ndani na wakawa hawawezi kufanya jambo lolote”.

Akabainisha kua: “Mwanadamu akitaka kitu anaweza kufanya ubunifu, ubunifu hutokana na kujiamini, ulimwengu wetu wa kiarabu unahitaji kiwango hicho cha umakini na kujiamini unaweza kufanya ubunifu, hususan sisi tunahistoria kubwa ya wanachuoni wengi walio kua na mchango mkubwa sana”.

Akamaliza kwa kusema: “Nadwa hii sio ya kuonyesha kilichopo, lakini tunataka kufaidika na kilichopo kwa lengo la kukiendeleza na kufanya ubunifu, na kujenga kujiamini kutokana na tulicho nacho, sawa sawa iwe katika sekta ya namba au maktaba, natarajia kuona ubunifu zaidi, tunaweza kufika viwango walivyo fika watu wengine au tukawazidi kabisa, wengi wanafahamu kua Atabatu Abbasiyya tukufu inategemea zaidi uwezo wa ndani, tuna amini uwezo wa ndani ni mkubwa na unaweza kufanya ubunifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: