Kutoka katika maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu rais wa umoja wa maktaba za kiarabu: kuanzishwa kwa mkakati wa kuendeleza maktaba za Iraq hadi mwaka (2030)…

Dokta Khalidi Halbiy
Rais wa umoja wa maktaba za kiarabu Dokta Khalidi Halbiy amesisitiza kua: “Hakika kufuta utambulisho wa taifa lolote huanzia katika kufuta turathi za kielimu na kitamaduni, hakika taifa bila utamaduni ni sawa na taifa bila utambulisho, yatupasa kua makini katika hili, wakati wote maktaba zipo hatarini, maktaba ngapi zimeshambuliwa na kuharibiwa kabisa katika ulimwengu wetu wa kiarabu na kiislamu, kinacho kusudiwa katika maktaba hizo sio karatasi zilizomo, bali ni utamaduni wa kiarabu na kiislamu, maktaba hizi ni amana kwetu lazima tuhakikishe tunazilinda na kuhifadhi turathi zetu”.

Aliyasema hayo katika ujumbe alio toa kwenye nadwa ya kielimu iliyo endeshwa na kituo cha faharasi na kupangilia maalumaat ambacho kipo chini ya maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, iliyo fanyika asubuhi ya Alkhamisi (28 Jamadal-Awwal 1439h) sawa na (15 Februari 2018m).

Akaongeza kusema kua: “Natoa shukrani za dhati kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na idara ya maktaba pamoja na daru makhtutwaat na kituo cha faharasi na kupangilia maalumaat kwa kunialika kuja kushiriki katika nadwa hii ya kielimu, napenda kuwafikishia salamu kutoka kwa wanachama wa umoja wa waarabu, pia nafurahi kua rais wa kwanza wa umoja wa maktaba za kiarabu ambae nimetembelea Iraq, hii ni ishara njema kwa maktaba za Iraq kua na mpango mkakati wa maendeleo hadi mwaka (2030) ulio anzishwa na umoja wa mataifa tangu mwaka (2015) na nchi ya Iraq ikausaini, Iraq itarudi kama ilivyo kua zamani”.

Akaongeza kau: “Hongera sana kituo cha faharasi na kupangilia maalumaat cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kutilia umuhimu jambo hili linalo beba dhana ya maendeleo endelevu na kulinda mazingira ya ubinadamu yanayo endana na uislamu pamoja na maelekezo ya Qur’an tukufu na maelekezo ya Mwenyezi Mungu mtukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: