Maoni katika picha
Mijadala ya nadwa ya siku ya pili ilisimamiwa na Dokta Jasim Jarjis kutoka chuo kikuu cha Marekani katika falme za kiarabu, na ilikua na mada kuu tatu, ambazo ni:
- - Mtazamo wa maendeleo endelevu katika kuandaa elimu ya maktaba hapa Iraq, iliyo wasilishwa na dokta Khalud Ali Arabi/ kutoka kitengo cha elimu na maktaba/ Juo kikuu cha Mustanswiriyya.
- - Nafasi ya maktaba katika kutoa maamuzi yatakayo pelekea kufanikiwa kwa mpango wa maendeleo wa Iraq, iliyo wasilishwa na Dokta Salman Judi Daud kutoka chuo kikuu cha Basra/ kitivo cha Adabu/ kitengo cha elimu na maktaba.
- - Taasisi za elimu za Iraq na changamoto za maendeleo endelevu katika mtazamo wa baadae, iliyo tolewa na Ustadh Jafari Hassan JaasimTwaaiy kutoka katika uongozi wa chuo kikuu cha Diyala/ katibu mkuu wa maktaba kuu.