Kamati ya maandalizi imeweka vigezo na kanuni za ushiriki katika shindano hili kama ifuatavyo:
- 1- Picha zipigwe kitaalamu na zionyeshe ushujaa wa Hashdi Sha’abi na jeshi la Iraq pamoja na matukio ya kibinadamu yanayo husu wakimbizi na maeneo yenye shida.
- 2- Mshiriki anaruhusiwa kushiriki kwa kuonyesha picha kati ya tano hadi kumi tu, na zisiwe na maandisi au jina.
- 3- Picha isibadilishwe kitu chochote wakati wa kushiriki.
- 4- Picha isiwe na alama za kivyama au kikabila na haikatazwi kua na alama ya Hashdi Sha’abi au bendera ya Iraq.
- 5- Picha inatakiwa kua na ukubwa wa (2000) hadi (3000).
- 6- Picha inatakiwa iwe iliyo pigwa na mshiriki mwenyewe.
- 7- Picha iwekwe kwenye albamu maalum ya mashindano ya fatwa ya ushindi na zipelekwe katika kitengo cha habari na utamaduni, au zikabidhiwe zikiwa katika (CD), pamoja na jina la mpiga picha, au zinaweza kutumwa kupitia barua pepe: (info@holyfatwa.com).
- 8- Haitakubaliwa picha yeyote ambayo haitakamilisha mashariti yaliyo tajwa.
- 9- Picha itakayo shiriki katika shindano, Atabatu Abbasiyya ndiyo itakayo kua na haki ya kuisambaza.
- 10- Mwisho wa kupokea picha ni (21 Juni 2018m).
- 11- Washindi watatu kwa kwanza watapewa zawadi ya hela kiasi cha (250,000) laki mbili na elfu hamsini dinari za Iraq kwa kila mmoja.