Atabatu Abbasiyya tukufu yatangaza shindano la filamu za Hashdi Sha’abi na yatoa wito kwa wataalamu waje kushiriki…

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda imetoa wito kwa wataalamu na wadau wa filamu waje kushiriki katika shindano la filamu zinazo onyesha ujasiri wanajeshi na Hashdi Sha’abi, litakalo fanyika katika kongamano linalo simamiwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kama sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya kutolewa kwa fatwa tukufu, chini ya kauli mbiu isemayo: (Ushindi umetokana na nyie ni wenu na nyie ndio mlioshinda) litakalo fanyika tarehe 13-14 Shawwal 1439h sawa na 28-29 Juni 2018m.

Kamati imeweka masharti yafuatayo ya ushiriki:

  • 1- Wazo la filamu liendane na kauli mbiu ya kongamano.
  • 2- Filamu ielezee ushujaa wa wanajeshi na Hashdi Sha’abi kwa ujumla katika kulinda kwao taifa na misingi ya ubinadamu, mazingira na maeneo matukufu.
  • 3- Isiwe imesha wahi kuonyeshwa katika mitandao au katika maonyesho mengine.
  • 4- Isizidi dakika ishirini na isiwe chini ya dakika moja, na iwe imetafsiriwa kwa kiengereza.
  • 5- Filamu itengenezwe katika aina ya (HD) au (Lavi).
  • 6- Ihifadhiwe kwenye (CD) na iwasilishwe katika kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na wasifu (CV) ya mtengenezaji wa filamu, au inaweza kutumwa kwenye mtandao huu (info@holyfatwa.com). Na mwisho wa kupokea filamu hizo ni (21 Juni 2018m).

Washindi watatu wa mwanzo watapewa zawadi za pesa kama ifuatavyo:

  • Mshindi wa kwanza: Milioni mbili dinari za Iraq (2,000,000).
  • Mshindi wa pili: Milioni moja na laki tano dinari za Iraq (1,500,000).
  • Mshindi wa tatu: Milioni moja dinari za Iraq (1,000,000).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: