Maoni katika picha
Ushiriki wa maonyesho haya ni miongoni mwa utaratibu wa ushiriki wa maonyesho ya kimataifa. Maonyesho haya sawa na maonyesho mengine, Ataba tukufu imekuja na zaidi ya aina (300) za vitabu vilivyo andikwa, kuhakikiwa na kuchapishwa na Ataba yenyewe, jambo ambalo halipo katika vituo vingine, jambo hili limekua likionyesha utofauti wao na vituo vingine katika maonyesho mengi ya kitaifa na kimataifa ambayo Ataba imeshiriki ikiwa ni pamoja na maonyesho haya.
Kumbuka kua maonyesho ya vitabu vya dini ya mwaka wa tano mfululizo yanafanyika sambamba na maonyesho ya vitabu ya kumi na tatu katika mji mtukufu wa Qum, maonyesho yeto mawili yatafanyika kwa muda wa siku kumi, kuanzia tarehe 15 hadi 25 Februari 2018, kukiwa na jumla ya taasisi na vituo vya usambazaji vinavyo shiriki (376) kutoka Iraq, Sirya, Uturuki, Jodan, Lebanon pamoja na Iran, kuna zaidi ya aina elfu themanini ya vitabu vikiwemo ambavyo vimeonyeshwa kwa mara ya kwanza.