Miongoni mwa mradi wa kitaifa wa kuandaa wasomaji: Maahadi ya Qur’an tukufu yahitimisha semina zake za kujenga uwezo…

Maoni katika picha
Miongoni mwa mradi wa kitaifa wa kuandaa wasomaji, kituo cha miradi ya Qur’an chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu cha Atabatu Abbasiyya kimemaliza semina ya kujenga uwezo, iliyo dumu siku kumi na tano na kuhudhuriwa na kundi kubwa la wasomaji, iliyo kua na wakufunzi mahiri kutoka ndani na nje ya Iraq.

Hafla ya kufunga semina ilifanyiwa katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kusomwa Qur’an ya ufunguzi ukafuata ujumbe wa Maahadi ya Qur’an tukufu ulio wasilishwa na mkuu wa Maahadi Shekh Jawaad Nasrawi, baada ya makaribisho na kuwapongeza wanafunzi walioshiriki, alisifu juhudi nzuri zinazo fanywa na kituo cha miradi ya Qur’an, alisema kua: “Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu tunahimiza sana kubobea katika kila fani, sawa sawa iwe katika ujenzi, elimu na vinginevyo, miongoni mwa vitu muhimu vinavyo stahiki kubobewa ni Qur’an, Maahadi ya Qur’an ni chombo pekee kinacho jihusisha na mambo ya Qur’an katika sekta zote na katika mikoa mingi ya Iraq, ambapo hushughulikia program za kuhifadhi Qur’an, usomaji wa Qur’an na maarifa ya Qur’an”.

Akaendelea kusema kua: “Kuhusu upande wa kuhifadhi na kusoma pamoja na miradi ya Qur’an kuna kituo maalum kinacho husika na harakati hizo nacho ni kituo cha miradi ya Qur’an, kimesha fanya harakati nyingi na miongoni mwake ni hii semina tunayo funga leo, semina hii ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kitaifa wa kuandaa wasomaji wa Qur’an wa Iraq, ulio pewa baraka na wasomi wakubwa wa Qur’an kutoka Misri, imeandaliwa kwa kufuata selibasi bora zaidi inayo simamiwa na walimu wa kimataifa walio bobea, katika semina hii wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali ya Iraq wamekutana katika mji mtukufu wa Karbala.

Hali kadhalika kulikua na ujumbe kutoka kwa mkufunzi wa kimataifa Abbasi Anjami kutoka Iran, ambae alimesema kua: “Hakika mafanikio haya na maendeleo mazuri tuliyo yaona kwa wanafunzi wa Iraq yamepita matarajio yetu, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tunatarajia kuiona Iraq kua nchi ya kwanza kwa Usomaji wa Qur’an, kutokana na juhudi tulizo ziona na uwezo mzuri wa vijana wake”.

Mwisho kabisa akasoma Qur’an Ahmadi Jamali mwanafunzi kutoka katika mkoa wa Dhiqaar, pamoja na kisomo kingine cha kikundi, baada ya hapo walimu wakapewa shahada za kutambua mchango wao kisha wanafunzi nao wakapewa shahada za ushiriki wa semina.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: