Kamati ya maandalizi ya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda yatangaza kufanyika kwa shindano la filamu fupi itakayo elezea ushujaa wa jeshi na Hashdi Sha’abi…

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda awamu ya tatu yatangaza shindano la filamu fupi na bora inayo onyesha ushujaa wa wanajeshi na Hashdi Sha’abi, na wametoa wito kwa wataalamu wajitokeze kushiriki katika shindano hilo litakalo fanyika katika kongamano litakalo simamiwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kama sehemu ya kuadhimisha kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda, chini ya kauli mbiu isemayo: (Ushindi umetokana na nyie ni wenu na nyie ndio washindi) litakalo fanyika tarehe 13 – 14 Shawwal 1439h sawa na 28 – 29 Juni 2018m.

Kamati imeweka mashariti yafuatayo ya kushiriki katika shindano hili:

  • 1- Wazo la filamu liendane na kauli mbiu ya kongamano.
  • 2- Filamu ionyeshe ushujaa wa wanajeshi na Hashdi Sha’abi kwa ujumla katika kulinda taifa, misingi ya ubinadamu, mazingira na maeneo matukufu.
  • 3- Isiwe imesha wahi kuonyeshwa katika vyombo vya habari au mitandao ya kijamii au imesha wahi kushiriki katika shindano lingine.
  • 4- Ihifadhiwe kwenye (CD) na iwasilishwe katika kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya pamoja na wasifu (CV) ya muandaaji, au itumwe kwenye barua pepe ifuatayo (info@holyfatwa.com).
  • 5- Mwisho wa kuzipokea ni (21 Juni 2018m).
  • 6- Isiwe chini ya dakika (3) na isizidi dakika (5).
  • 7- Iwapo itaelezea mambo ya kihistoria yawe matukio halisi.
  • 8- Kama kuna mateso na umwagaji wa damu wa kikatili visionyeshwe moja kwa moja.

Washindi watatu wa kwanza watapewa zawadi ya pesa kama ifuatavyo:

  • Mshindi wa kwanza: Milioni moja dinari za Iraq (1,000,000).
  • Mshindi wa pili: Laki saba na elfu hamsini dinari za Iraq (750,000).
  • Mshindi wa tatu: Laki tano dinari za Iraq (500,000).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: