Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu atembelea kituo cha Alkafeel cha uchapishaji na utengenezaji wa mabango na apongeza juhudi za watendaji wake…

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amepongeza utendaji wa wataalamu wa kituo cha uchapishaji cha Alkafeel kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na maendeleo yaliyopo katika utendaji wake, sambamba na juhudi za Ataba tukufu za kuhakikisha kila kitengo kinapata vitendea kazi vyake na kuviwezesha kupanga na kushiriki katika maonyesho, makongamano, nadwa pamoja na harakati zingine.

Yalisemwa hayo alipo tembelea kituo tajwa hapo juu ambapo alifuatana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Muhandisi Muhammad Ashiqar, walisikiliza maelezo kutoka kwa mkuu wa kituo Ustadh Muhammad Aali Taajir, kuhusu utendaji wao na vifaa vya kisasa walivyo navyo, kikiwemo kifaa cha kisasa zaidi cha namba, ambacho ndio cha kisasa zaidi kuingia hapa Iraq, Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria amehimiza umuhimu wa kujiendeleza kielimu na kuendelea kufanya vizuri, na akatoa wito wa kufanya kazi kwa bidii na kwa tim.

Kumbuka kua kituo cha uchapishaji cha Alkafeel ni moja ya vituo vya kitaalamu na kinamajukumu mengi, miongoni mwa majukumu yake ni:

  • - Kusanifu na kuandaa vipeperushi vinavyo endana na mazingira ya kongamano au maonyesho na kwa muonekano mzuri unao lingana na hadhi ya tukio na sehemu husika.
  • - Kusanifu na kuchapisha kadi za mialiko.
  • - Kusanifu na kuandaa zawadi, midani na shahada za aina mbalimbali na ukubwa tofauti.
  • - Kusanifu na kutengeneza majukwaa ya matangazo.
  • - Kuandaa misafara ya matangazo ya mradi wowote wa Atabatu Abbasiyya kwa kufuata utaratibu wa mradi husika.
  • - Kupangilia matukio na harakati zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, makongamano na maonyesho pamoja na kufanya shughuli zote za kiutumishi na kiratiba.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: