Maoni katika picha
Mlango wa Kibla katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umeshuhudia kuwekwa kwa bango kubwa lililo funika sehemu ya mbele ya mlango huo, lenye urefu wa (mita 26) na upana wa (mita 6) limedariziwa kwa rangi nyeupe neno lisemalo (Amani iwe juu yako ewe Swidiqatu Shahidah) na pembeni ya neno hilo kuna neno lingine lisemalo (Ewe Fatuma Zaharaa).
Bango lingine limewekwa katika mlango wa Imamu Hassan (a.s) likielekezwa upande wa uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, lenye urefu wa (mita 16) na upana wa (mita 6) likiwa limedarizwiwa neno lisemalo (Amani iwe juu yako ewe Swidiqah Shahidah) kwa rangi nyekundu, na kuna neno lingine lisemalo (Ewe Fatuma Zaharaa) na pembezoni mwake kumeandikwa (Reihanatu Nabi) kwa rangi ya kijani ikiashiria bibi Zaharaa (a.s).
Atabatu Abbasiyy tukufu kama kawaida yake kila mwaka, imeandaa ratiba ya taazia yenye shughuli nyingi za kimaombolezo, kama vile utoaji wa mihadhara ya kidini, kufanyika kwa majlis za maombolezo kwa ajili ya kuadhimisha tukio hilo, pia wametangaza utayali wao wa kupokea mawakibu za maombolezo kutoka ndani na nje ya mji mtukufu wa Karbala wanaokuja kutoa taazia kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Fahamu kua hakuna tarehe kamili ya kifo cha bibi Fatuma Zaharaa (a.s), hivyo waumini wa duniani kote hufanya kumbukumbu ya kifo chake katika siku tofauti, kutokana na kutofautiana kwa riwaya, kipindi cha mapmbolezo hayo huitwa (kipindi cha huzuni za Fatwimiyya).