Idara ya makhatibu wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendesha semina ya kujenga uwezo kwa jopo la makhatibu wa mimbari ya Husseiniyya, kwa ajili ya kuchangia kuboresha mihadhara katika uzungumzaji na njia za kuwasilisha, pamoja na vitu vingine vinavyo weza kusaidia kufikisha ujumbe wa Imamu Hussein (a.s) kwa makundi yote ya jamii na kwa viwango tofauti.
Hii ni moja ya semina zinazo fanywa na idara hii katika mwaka, kufuatia utaratibu wake wa kuongeza wataalamu, na kuwaongezea maarifa yatakayo ongeza kiwango chao cha uzungumzaji, katika semina hii amealikwa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Muhsin Hakim kutoka katika mji mtukufu wa Qum.
Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara: “Semina hii ina jumla ya washiriki (200) wakiume na wakike, zimetumika kumbi mbili katika semina hii, ukumbi wa Sayyid Auswiyaa wa Atabatu Husseiniyya tukufu na makao makuu ya idara ya makhatibu wa kike yaliyopo katika shule ya Darul-Ilmi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, zimefundishwa mada nyingi, mada zote zinalenga kufundisha njia bora ya kufikisha ujumbe wa Imamu Hussein katika jamii kwa namna ambayo inaendana na mazingira ya tabligh ya zama zetu, pamoja na kubainisha majukumu ya makhatibu katika kupambana na hujuma za kifikra na ki-itikadi zinazo fanyiwa dini ya kiislamu kila wakati”.
Akaongeza kusema kua: “Hali kadhalika walielezewa umuhimu wa kushikamana na misingi ya lugha ya kiarabu, na kutumia rejea zinazo kubalika katika kuandaa mada na kufuata utaratibu mzuri katika kuwasilisha bila kua na taasubu, pamoja na namna ya kuongea wakati wa uwasilishaji wa mada”.
Kumbuka kua sababu ya kuanzishwa kwa idara hii ni kwa ajili ya kuimarisha tabligh katika sekta ya wanawake kutokana na umuhimu wao hasa katika kibindi cha maombolezo, na kuwatoa katika uwanja mdogo na kuwapeleka katika uwanja mpana watakao weza kuelezea swala la Imamu Hussein kwa njia zinazo eleweka na zinazo endana na uhalisia.