Shule za Alkafeel za wasichana zakusudia kufanya kongamano la (Ruuhu Nubuwwah) awamu ya pili na zasisitiza kua litakua la aina yake…

Maoni katika picha
Idara ya shule za Alkafeel za wasichana iliyo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza azma yake ya kufanya awamu ya pili ya kongamano la (Ruuhu Nubuwwah) chini ya kauli mbiu isemayo: (Fatuma “a.s” ni kheri iliyo eneo na tunda la peponi) litakalo fanyika kwa ajili ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s), kongamano hilo hua ni mahala pa kujifunza fikra na tamaduni zake (a.s), wakasisitiza kua litakua la aina yke, kwa sababu maandalizi yameanza mapema jambo linalo endana na tukio hili.

Mkuu wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo, Ustadhat Bushra Jabbaar amesema kua: “Maandalizi ya kongamano hili yanaendelea na yamefikia mahala pazuri, tayali tumesha gawa majukumu ya kongamano kwa vitengo vidogo vidogo, kama vile kitengo cha Zainabiyaat idara ya maktaba ya wanawake na idara ya redio, shule za Ameed na Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya kitengo cha maarifa pamoja na idara ya kituo cha swidiqah na watumishi wake”.

Akasema kua: “Kamati zinafanya kazi kwa kujituma na hamasa kubwa kwa ajili ya kumtumikia muhusika wa tukio, kongamano hili linatarajiwa kua la aina yake tofauti na kongamano lililo pita kutokana na kua na muda wa kutosha wa maandalizi, na maandalizi yanaendelea vizuri katika nyanja zote, pia mwaka huu imeundwa kamati maalum ya wasomi, muaustadhat tisa kutoka vyuo vikuu watakao kagua mada zitakazo wasilishwa katika kongamano”.

Bushra akabainisha kua: “Nchi zitakazo shiriki katika kongamano hili mwaka huu hadi sasa zimesha zidi kumi wakati mwaka jana zilikua nchi sita tu”.

Kumbuka kua lengo la kufanya kongamano hili ni kuonyesha nafasi ya bibi Zaharaa (a.s) katika mambo mbalimbali, na kuondoa pazia kuhusu mchango wake kifikra kupitia mada zitakazo wasilishwa, na kuingiza vitabu katika maktaba kuhusu mtu huyu mtakasifu na athari yake kifikra ndani ya jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: