Jopo la wahandisi wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) waondoa vifaa vya kivita na mabomu ya kutega ardhini katika eneo kubwa ndani ya mkoa wa Barsra…

Maoni katika picha
Katika opresheni ya “Wafaau Kubra” inayo fanywa na kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) brugedi ya wahandisi, wamesafisha eneo kubwa pamoja na njia mbalimbali katika mkoa wa Basra, zilizo kua na mabaki ya vifaa vya kivita na mabomu ya kutegwa ardhini yaliyo pelekea vifo vya watu na wengine wengi kujeruhiwa.

Uondoaji wa mabaki hayo ya vifaa vya kivita umefanyika kwa kutumia kifaa cha kisasa kabisa katika kazi hiyo ambacho ni (scanjack), kituo cha kwanza cha kazi hii kilikua katika mji wa mpakani Shalamija katika wilaya ya Shatul-Arabu pamoja na miji inayo pakana na mji huo, iliyo kua na maeneo kamubwa yaliyo kua yamejaa mabaki ya vifaa vya kivita.

Kumbuka kua opresheni hii tukufu ilipewa baraka na Marjaa dini mkuu kupitia ulimi wa mwakilishi wake Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ilihusisha kuondoa vifaa vya kivita pamoja na miradi mingine, pia haijafanyika katika mkoa wa Basra peke yake, kuna opresheni zingine zimefanyika katika mkoa wa Swalahu Dini kwa kufuata utaratibu kama ulivyo pangwa, kikosi kinafanya kila kiwezalo kwa ajili ya kuhakikisha kazi hii inaendelea kwa mafanikio.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: