Msafara wa Saaqi watoa ratiba ya pili ya ibada ya Umra katika mwaka 1439h /2018m...

Maoni katika picha
Idara ya kunufaika na mitambo ya Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia msafara wake wa Saaqi awamu ya pili imetangaza ratiba mpya ya safari ya kwenda Umra na kuzuru kaburi la Mtume (s.a.w.w) pamoja na Maimamu wa Baqii (a.s) na sehemu zingine tukufu katika mji wa Maka na Madina, wanatoa huduma bora zaidi ya chakula, malazi na usafiri.

Msafara wa Saaqi tangu walipo anza safari za kwenda katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu wamekua wakitoa huduma bora zaidi kwa wateja wao.

Ratiba za safari zipo kama ifuatavyo:

  • 1- Safari ya nusu ya mwezi wa Jamadal-Thani, kuanza safari (06/03/2018m, sawa na 17 Jamadal-Thani).
  • 2- Safari ya mwanzoni mwa mwezi wa Rajabu, kuaza safari (20/03/2018m, sawa na 2 Rajabu).
  • 3- Safari ya Shaabaniyya, kuanza safari (11/04/1018m, sawa na 24 Rajabu).
  • 4- Safari ya nisu ya mwezi wa Shabani, kuanza safari (27/04/2018 sawa na 10 Shabani).
  • 5- Safari ya mwisho wa mwezi wa Shabani, kuanza safari (12/05/2018m, sawa na 25 Shabani).

Ratiba inahusisha vitu vifuatavyo:

  • 1-
  • 2- Kukaa siku nne Madina na siku sita Maka.
  • 3- Kutembelea maeneo matukufu katika mji wa Madina.
  • 4- Katika mji wa Madina na Maka watakaa katika hoteli nzuri zaidi.

Siku ya kwanza: Kukusanyika katika kituo cha Saaqi kwenye barabara ya Maitham Tammaar kwa ajili ya kwenda uwanja wa ndege na kuanza safari ya kwenda Madina, baada ya kufika Madina watapewa vyumba hotelini na kulala.

Siku ya pili: Kutembelea msikiti Mtukufu wa Mtume na Maimamu wa Baqii (a.s).

Siku ya tatu: Kutembelea maeneo matukufu ya Madina, ikiwa ni pamoja na kaburi la Hamza (a.s), mashahidi wa Uhudi, Masjid Qiblataini, Masaajid Sab’a –misikiti saba- Masjid Kubba kisha tutaenda katika bustani ya watumishi wa Hassan (a.s) kwa ajili ya kutabaruku (kula) chakula.

Siku ya nne: Kupumzika na kutembea madukani.

Siki ya tano: Kujiandaa na kuondoka baada ya Adhuhuri kwenda Miqaat kwa ajili ya Ihraam kwenye Masjid Shajara, na kuondoka hapo baada ya Magharibi kwenda Maka, baada ya kufika Maka watapewa vyumba na kulala.

Siku ya sita: Kufanya ibada ya Umra.

Siku ya saba: Kupumzika.

Siku ya nane: Kutembelea maeneo matukufu ya Maka (Jabal Thuur, Arafaat, Muzdalifa, Mina, Jabal Nuur na makaburi ya Hajuun).

Siku ya tisa: Kufanya umra kwa niaba kwa watakao penda kufanya hivyo.

Siku ya kumi: Kupumzika.

Siku ya kumi na moja: Kurudi katika nchi yetu kipenzi na kufika salama tukiwa na kheri nyingi InshaAllah.

Gharama za kushiriki katika safari hizi ni:

  • 1- Mtu mwenye umri wa miaka (12 na zaidi) keshi ni ($850) na kwa mkopo ni ($950).
  • 2- Mtoto mwenye umri wa miaka (2 – 11) keshi ni ($500) na mkopo ni ($600).
  • 3- Mtoto anaye nyonya mwenye umri chini ya miaka (2) keshi ni ($150) na mkopo ni ($600).
  • 4- Malipo ya chumba cha pili kwa anayetaka ni ($200).

Zingatia:

  • 1- Msafara utafuatana na kiongozi wa idara pamoja na muelekezaji wa mambo ya dini.
  • 2- Kila siku watatoa milo mitatu katika kipindi chote cha safari.
  • 3- Anaye taka kwenda Umra awasilishe paspoti ambayo bado inaendelea kutumika kwa zaidi ya miezi sita pamoja na kitambulisho chake cha uraia na picha tatu ndogo (paspot saizi).
  • 4- Anaye taka kwenda Umra kwa mkopo lazima apate mdhamini ambaye ni mtumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, deni lake litalipwa kwa kukata mshahara unaolipwa na Alkafeel, pia anatakiwa atangulize ($200) na atakatwa kila mwezi ($100) kutoka kwenye mshahara.
  • 5- Mkopo wa mtoto mwenye umri wa (2 – 11) atatanguliza ($100) na atakatwa kila mwezi ($50).

Kwa maelezo zaidi au kupata nafasi tembelea ofisi ya kunufaika na mitambo ya Atabatu Abbasiyya tukufu iliyopo katika mlango wa Bagdad karibu na kizuwizi cha Qamar katika hoteli ya Aljazira ya zamani. Au piga simu namba zifuatazo: (07801952463 / 07602283026).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: