Kuongeza muda wa usajili na kushiriki katika shindano la milango ya rehma photograph…

Maoni katika picha
Kamati inayo simamia shindano la milango ya rehma, linalo husika na kupiga picha milango ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) litakalo simamiwa na kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya, imetangaza kuongeza muda wa usajili wa kushiriki, kwa ajili ya kutoa nafasi zaidi kwa washiriki, sasa mwisho wa kujisajili utakua (10 Machi) na siku ya kupiga picha itakua (13 Machi) na siku ya mwisho ya kuwasilisha picha itakua (16 Machi 2018m), kamati imesisitiza kua tarehe hizo ni za mwisho hazitabadilishwa tena, washindi watajulishwa kupitia mawasiliano na watu wote watakao shiriki watapewa vyeti vya ushiriki.

Kamati imefafanua masharti ya shindano hili kama ifuatavyo:

  • 1- Kujisajili kwa ajili ya ushiriki kutafanyika kupitia mtandao ufutao: (https://alkafeel.net/alrahma).
  • 2- Mpiga picha aliye sajiliwa atapewa kitambulisho (baji).
  • 3- Washiriki watakusanyika katika kitengo cha miradi ya kihandisi, kilichopo mwanzoni mwa barabara ya Alqami upande wa Atabatu Abbasiyya tukufu (hoteli ya Aali Yasini ya zamani) katika siku zilizo tajwa hapo juu, kuanzia saa moja asubuhi hadi saa saba Adhuhuri kwa ajili ya kuchukua vitambulisho (baji) na kukamilisha taratibu zote za ushiriku.
  • 4- Mpiga picha anahaki ya kupiga picha milango iliyo ongezwa katika Atabatu Abbasiyya peke yake.
  • 5- Faili zitakabidhiwa kwa namba, picha ziwe na upana wa (3600) na ubora wa (dpi300).
  • 6- Picha zitapokelewa kupitia mtandao huu (https://alkafeel.net/alrahma) au kwa kuziwasilisha moja kwa moja katika ofisi ya kitengo cha miradi ya kihandisi iliyopo mwanzoni mwa barabara ya Alqami upande wa Atabatu Abbasiyya tukufu (hoteli ya Aali Yasini ya zamani).
  • 7- Mpiga picha anaruhusiwa kufanya marekebisho ya rangi na mwanga, haitakubaliwa bicha itakayo fanyiwa mabadiliko makubwa hadi ikapoteza sifa ya kua picha ya photograph.
  • 8- Haitakubaliwa picha yeyote itakayo kua na jina au nembo maalumu.
  • 9- Picha zitakazo kubaliwa ni zile zitakazo pigwa wakati wa shindano tu.
  • 10- Baada ya washiriki kukabidhi picha katika kamati ya shindano, picha hizo zitakua chini ya umiliki wa kitengo cha miradi ya kihandisi na watakua na haki ya kuzirudufu na kuzitumia katika miradi yao.

Kamati ya maandalizi ya shindano imeandaa zawadi ya pesa zifuatazo:

  • Mshindi wa kwanza: (1,000,000) milioni moja, dinari za Iraq.
  • Mshindi wa pili: (500,000) laki tano, dinari za Iraq.
  • Mshindi wa tatu: (250,000) laki mbili na elfu hamsini, dinari za Iraq.
  • Mshindi wa nne hadi wa kumi: (150,000) laki moja na elfu hamsini, dinari za Iraq.

Kumbuka kua shindano hili ni kwa ajili ya kuonyesha mafanikio makubwa waliyo pata mafundi na wahandisi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika miradi yao, ukiwemo mradi wa kutengeneza milango ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mradi ambao ni kielelezo bora cha ubunifu na ufundi wa raia halisi wa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: