Ofisi ya wanawake ya Atabatu Abbasiyya tukufu yahitimisha ratiba ya (kitabu ni rafiki yangu) na yasisitiza kua walifikia malengo na walipata mwitikio mkubwa…

Maoni katika picha
Idara ya ofisi ya wanawake ya Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha ratiba ya (kitabu ni rafiki yangu) iliyo tekelezwa katika program ya (marafiki wa maktaba na wapenzi wa utamaduni) iliyo fanyika kipindi cha likizo, na kushiriki kundi kubwa la wanafunzi wa shule za sekondari pamoja na wa shule za dini na wadau wa maktaba.

Kiongozi wa idara Ustadhat Asmaa amesema kua: “Kwa ufupi ratiba hii ililenga kushajihisha usomaji kwa vitendo katika nyoyo za washiriki, jambo hili linafaida kuu mbili, kwanza: Kuelewa malengo ya kitabu na kukifanyia kazi katika jamii. Pili: Kutengeneza kizazi kinacho weza kuelewa malengo ya kitabu na kukifanyia mukhtasari”.

Akabainisha kua: “Kwa ujumla ratiba ilikua na mafanikio makubwa, miongoni mwa vitu vilivyo pata mwitikio mkubwa ni ratiba ya (kitabu ni rafiki yangu) ambayo ilisimamiwa na idara ya kusaidia usomaji kwa kushirikiana na idara ya kuazimisha, kwa pamoja waliwajibika kusimamia ratiba hiyo”.

Naye Ustadhat Aalaa Khafaaf kutoka katika afisi ya kusaidia usomaji na uwasilishaji amesema kua: “Program hii ni jambo zuri kwa wanafunzi, kwani inawapa msukumo wa kujisomea, na imekua na mwitikio mzuri, kutokana na utafiti wetu tumebaini kua, wanafunzi wengi wamenufaika sana na vitabu vilivyopo, na hii ndio ndoto ya kila mradi wenye mafanikio, kwa kweli tunahitaji zaidi miradi ya aina hii, kwa sababu inajenga moyo wa kusoma vitabu katika kipindi hiki ambacho teknolojia imejaa katika jamii, mimi naichukulia program hii sawa na taa linalo angazia njia watembeaji waliopo katika giza nene”.

Akaendelea kusema kua: “Kuhusu utekelezaji wa mradi huu, tunaweka vitabu sehemu maalumu ili iwe rahisi kwa washiriki kuchagua aina ya kitabu anacho hitaji kuazima, kisha yanaandikwa maelezo ya mwanafunzi, (jina la kutabu kinacho azimwa, jina la muazimaji, jina la shule anayo soma au taasisi anayo toka na namba ya simu kama anayo), baada ya kuchukua kitabu na kukisoma anaandika muhtasari ndani ya muda ulio pangwa, na tumejitahidi kubadilisha utaratibu tofauti na wazamani”.

Kumbuka kua program hii na mradi huu unatekelezwa kutokana na ukweli kua kusoma ndio njia nzuri ya kukomaza akili na kuipa elimu mbalimbali, baada ya kuja mitandao ya kijamii ya kisasa imechangia kwa kiasi kikubwa kushusha moyo wa kujisomea, ndipo Atabatu Abbasiyya tukufu ikakusudia kuhimiza usomaji na kujenga moyo wa kujisomea kwa kutumia program maalum, inayo husisha mashindano na kutoa zawadi ili kuwapa moyo wanafunzi, na kumfanya kila mmoja miongoni mwao awe ni rafiki wa maktaba, na aweze kuelezea alicho kisoma kwa namna anayo penda mwenyewe (kwa kuandika muhtasari, kuchora, kuelezea kisa au kwa njia ya shairi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: