Mjini Cairo kwa mara ya kwanza katika kiwango cha Ataba tukufu: Maktaba ya Atabatu Abbasiyya yafanya maonyesho ya vitu nadra na nakala kale…

Maoni katika picha
Ushiriki wa makta na Daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu hauja ishia katika kongamano la pili la (Turathi tukufu za kiarabu na kiislamu na vitendo vya kitamaduni) chini ya wenyeji wa Maahadi ya nakala kale za kiarabu katika jiji la Cairo (Al-Alaksu), ambayo yameandaliwa kwa kushirikiana na: Maahadi tajwa, kituo cha kuhakiki nakala kale katika chuo kikuu cha Qanaat Sawis, na kituo cha kuhuisha turathi za kielimu katika chuo kikuu cha Bagdad, katika upande wa utafiti, pia kulikua na harakati zingine zilizo kamilisha huu ushirikiano, kufuatia kufanya maonyesho ya vifaa kale na baadhi ya vitabu, ambapo kilishiriki kituo cha upigaji picha wa nakala kale na faharasi, na kituo cha Abulfadhil Abbasi (a.s) cha ubobezi katika masomo pamoja na kituo cha kuhuisha turathi katika idara ya maktaba.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyo tolewa kwa mtandao wa kimataifa Alkafeel na kiongozi wa ujumbe huo Ustadh Swalahu Mahdi Abdulwahabi, amesema kua: “Maonyesho haya yanafanyika kwa mara ya kwanza katika kiwango cha Ataba tukufu za Iraq na ulimwengu wa kiislamu, na imekua fursa nzuri ya kutambulisha na kubainisha vitu vinavyo milikiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu miongoni mwa hazina tukufu za turathi, pamoja na juhudi kubwa wanayo fanya ya kuzikarabati na kuhakikisha zinakua katika muonekano wake halisi kwa ajili ya kunufaika nazo”.

Akaongeza kusema kua: “katika maonyesho haya tumeonyesha jumla ya nakala kale (32) ambazo historia yake inarejea karne ya kwanza hijiriyya hadi karne ya kumi na tatu hijiriyya, na jumla ya vitabu vilivyo onyeshwa ni (40), miongoni mwa vitabu hivyo vipo vilivyo hakikiwa na vipo vilivyo tungwa, pamoja na kuonyesha sambuli mbali mbali za pete kutoka katika maktaba za Iraq za kiarabu na kiajemi”.

Akabainisha kua: “Hakika kila kituo kimeshiriki kwa kuonyesha vitu vyake, kituo cha upigaji picha nakala kale na faharasi kimeonyesha msahafu mtukufu ambao historia yake inarejea karne ya kwanza hijiriyya hadi karne ya kumi na tatu hijiriyya, na picha ya kihistoria iliyo ishi miongo mingi katika historia ya kiislam, pamoja na ubao wa picha ya ardhi ya Sharifu Idrisa ambayo ni ya karne ya sita hijiriyya, pia wameonyesha machapisho mbalimbali ya kituo, kama vile faharasi za nakala kale na msahafu ulio hakikiwa wa ibun Bawwaab”.

Akasema kua: “Kituo cha Abulfadhil Abbasi (a.s) cha ubobezi wa masomo kimeonyesha sehemu ya vitabu vilivyo andikwa na kituo hicho, yakiwemo majarida kuhusu historia ya mwezi wa bani Hashim (a.s), pamoja na vitabu vingine vinavyo muelezea Abulfadhil Abbasi (a.s), na kituo cha uhuishaji wa turathi kilikua na bidhaa nyingi za kuonyesha, miongoni mwa bidhaa zake ni kitabu cha: (Aqrabu Majazaat) na (Majallatul-Khazaanah) pamoja na vitabu vingine vinavyo tokana na utafiti na uhakiki wa nakala kale, pamoja na kuonyesha sehemu ya kazi za uhakiki walizo fanya”.

Ustadh Swallaahu akamaliza kwa kusema kua: “Maonyesho haya yamepongezwa na wahudhuriaji pamoja na washiriki kutoka nchi mbalimbali na wamefurahishwa sana”.

Kumbuka kua maonyesho haya ni sehemu ya orodha ndefu ya maonyesho ambayo maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu wameshiriki, kwa ajili ya kubainisha na kuonyesha vitu vilivyopo katika Ataba tukufu katika sekta hii, ambavyo wamevifanya na kuviandaa kwa ajili ya kulinda turathi, na kuporesha uhusiano kati yake na taasisi zingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: