Uongozi mkuu wa Atabatu Husseiniyya na Abbasiyya umeratibu matembezi makubwa ya kushindikiza kimaigizo kwa mashahidi wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi…

Maoni katika picha
Chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) na kwa kushiriki Mawakibu Husseiniyya zao alasiri ya Juma Mosi (7 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (24 Februari 2018m) wameshindikiza majeneza ya kimaigizo ya mashahidi wa Iraq walio loanisha ardhi hii damu zao tukufu na wakaondoa hatari ya magaidi wa Daesh, na wakafanya vitimbi vya magaidi viwarudie wenyewe na wakatibua njama zote zilizo kusudia kuleta shari katika nchi ya Mahdi na mitume.

Ushindikizaji wa jeneza la kimaigizo ulianzia katika barabara ya Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakiwa wamebeba bendera za Iraq na za vikosi vya Hashdi Sha’abi, wakitanguliwa na jeneza la kuigiza huku ikipigwa mimbo ya kuomboleza, wakatembea hadi katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu ambapo kilifanyika kikao cha kuomboleza kilicho hudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na mkuu wa mkoa wa Karbala na viongozi wa Hashdi Sha’abi.

Baada ya kusomwa Qur’an ya ufunguzi na kusoma surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq na Hashdi Sha’abi, ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) ulio wasilishwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar ambaye alisema kua: “Pongezi kubwa kwa walio shiriki, wakachangia, wakajitolea, wakapata shahada chini ya bendera ya Iraq na kivuli cha fatwa tukufu ya kuilinda ardhi na maeneo matukufu, hongeza sana kwa familia zao na watoto wao kwa kupata utukufu huu mkubwa wa kufuata nyayo za maimamu watakasifu (a.s)”.

Ukafuata ujumbe wa Hashdi Sha’abi ulio wasilishwa kwa niaba yao na kiongozi wa kamati ya habari katika mkoa mtukufu wa Karbala Ustadh Maidham Atabi ambae amesema kua: “Kuwakarimu kwa kweli na kuwapongeza pamoja na kuwakumbuka na kuwapa heshima ya kweli (mashahidi wetu watukufu) tunatakiwa kusaidia familia zao zilizo jitolea kila kilicho bora katika maisha yao bila kutafuta sifa wala malipo yeyote, hakika hawa ni watu watukufu sana kwetu sote, yatupasa kujifunza kutoka kwao somo ya subira na kujitolea…”.

Kisha ukafuata ujumbe wa rais wa kitengo cha Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya bwana Riyadh Niimah Salmaan, miongoni mwa aliyo sema ni: “Kutoka katika ardhi ya shahada na kujitolea, tukiwa karibu na Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) leo tumeshindikiza jeneza la kuigiza la mashahidi wa Iraq miongoni mwa wanajeshi wa serikali na Hashdi Sha’abi, ipo wazi kwenu kwamba ardhi hii tukufu inaupekee maalum, ni ardhi ya shahada na kujitolea inaonganisha harakati za zamani na za sasa, hapa ndipo alipo simama Imamu Hussein (a.s) kupambana na waovu katika kizazi cha Abusufiyani na Aali Marwan na vibaraka wao, waliotaka kufuta mafundisho ya dini na kuzima nuru ya utume katika vita ya Twafu ya milele, amabyo damu ilishinda upanga na Karbala imekua taa liangazalo na bendera ipepeayo”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika Imamu Hussein (a.s) aliweka jiwe la msingi katika kupambana na waovu, baada ya miaka 1400 wamerudi tena waovu na kutaka kufanya ufisadi katika Umma wa kuangamiza watu na mimea, kwa kua Mwenyezi Mungu amewatukuza wapiganaji wa jihadi zaidi ya waliokaa (bila kugigana jihadi) na akaifanya jihadi kua ni mlango miongoni mwa milango ya pepo, ilitolewa fatwa ya jihadi kifai katika mazingira magumu, iliyo kua na maneno matukufu yenye maana kubwa na siri nzito, fatwa iliyo weza kubadilisha historia ya sasa, na kubadilisha vipimo vya nguvu vya kieneo na kimataifa, likatokea jambo kubwa lililoifanya dunia izindike na kuitambua hatari kubwa inayo ikabili, uchawi ukamrudia mchawi mwenyewe, fatwa ikaonyesha mazingira halisi ya imani ya Maimamu (a.s) na ikafikia malengo yake, natoa shukrani kubwa kwa watu wote mlio hudhuria na ninawatakia rehma na amani mashahidi wetu watukufu, Mwenyezi Mungu awaponye haraka majeruhi wetu na awaangamize maadui wa Iraq”.

Shughuli hii ilipambwa na qaswida za kimashairi na semi za husseiniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: