Zaidi ya bilioni tatu na nusu thamani ya huduma za kitabibu za bure zilizo tolewa na hospitali ya rufaa Alkafeel…

Maoni katika picha
Kutokana na maelezo yaliyo pewa mtandao wa kimataifa Alkafeel, mkuu wa hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu dokta Haidari Bahadeli ametangaza kiwango cha thamani ya huduma za kitabibu zilizo tolewa bure, zimefika zaidi ya dinari bilioni tatu na nusu ndani ya miaka miwili tu, huduma huzo zilitolewa kwa makundi mbalimbali ya watu, likipewa umuhimu zaidi kundi la mafakiri, masikini, familia za mashahidi wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi pamoja na watu waliopata majeraha vitani.

Akaongeza kusema kua: “Tangu kufunguliwa kwa hospitali hii, na kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, imepiga hatua kubwa katika jambo hili (la kutoa huduma bure) na imeweka utaratibu wa kuwapokea na kuwapa huduma”, akasisitiza kua: “Hospitali bado inaendelea kutoa huduma ya matibabu ya bure kwa makundi ya watu tuliyojata kwa kufuata utaratibu uliowekwa unao endana na ongezeko la watu hao”.

Akabainisha kua: “Huduma zilizo tolewa bure ni upasuaji wa aina zote, uwekaji wa hema za matimabu, na sehemu nyingine ilikua ni punguzo la bei, wanufaika wa huduma hii hupokelewa kupitia taasisi za kijamii na kibinadamu za ndani na nje ya mkoa mtukufu wa Karbala”.

Bahadeli akabainisha kua: “Huduma za bure hazitolewi ndani ya hospitali peke yake, bali kuna misafara ya kutoa huduma za matibabu inayo fanywa na madaktari wake ikiwa ni pamoja na mradi wa (matibabu bila malipo), unaolenga miji na vijiji vyenye upungufu wa huduma za matibabu, ambapo madaktari wetu bingwa na wauguzi huweka kambi na kutoa huduma za matibabu bure na wenye matatizo makubwa huwapeleka hospitali kwa matibabu zaidi”.

Akasisitiza kua: “Kiwango cha pesa inayo tumika kwa ajili ya utoaji wa huduma za kimatibabu, kulipia maji na umeme kwa wizara ni kikubwa sana, ukiongeza na pesa za mishahara ya madaktari, wauguzi na watumishi wengine tunao wapokea kutoka katika nchi za kiarabu na kiajemi kwa ajili ya kuwatumikia raia wa Iraq, bila kusahau vifaa tiba vya kisasa ambavyo vimesaidia kutuwezesha kutoa huduma bora kwa wagonjwa ndani ya Iraq, na kuwafanya wananchi wa Iraq wasisafiri kwenda nje ya nchi kutafuta matibabu, mambo yote hayo yanagharama kubwa ambayo inafanya iwe haiwezekani hospitali kutoa huduma bure mia kwa mia”.

Kwa maelezo zaidi au kuangalia huduma zinazo tolewa na hospitali unaweza kuingia katika mtandao wa hospitali ambao ni: www.kh.iq au piga simu zifuatazo: (07602344444 / 07602329999).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: