Kamati iliyo simamia kongamano la Ruhu Nubuwah yatangaza majina ya tafiti zilizo faulu katika shindano la utafiti…

Maoni katika picha
Kamati iliyo simamia kongamano la kimataifa la Ruhu Nubuwah la mwaka wa pili linalo endeshwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya shule za dini za wasichana Alkafeel, imetangaza majina ya tafiti zilizo faulu katika shindano la utafiti kama ifuatavyo:

Mshindi wa nafasi ya kwanza:

Jina la utafiti: Utetezi wa bibi Zaharaa (a.s) kuhusu mwenendo wa Uimamu.

Jina la mtafiti: Shimaa Yasi Al-Aamiriy na Narjis Karim Khadhiri – Iraq.

Mshindi wa nafasi ya pili:

Jina la utafiti: Zana za utetezi za bibi Zaharaa (a.s) katika kupambana na dhulma na madhalimu: Maana ya Munahadha kilugha na ki-istilahi.

Jina la mtafiti: Hindu Faadhil Abbasi – Iraq.

Mshindi wa nafasi ya pili:

Jina la utafiti: Nafasi ya bibi Zaharaa (a.s) na utukufu wake katika hadithi za Mtume (s.a.w.w) na Maimamu watakasifu.

Jina la mtafiti: Mina Ibrahim Muhammad Shekh Ahmadi – Baharain.

Mshindi wa nafasi ya tatu:

Jina la utafiti: Nadhariya ya Hijabu baina ya bibi Zaharaa (a.s) na Qur’an tukufu.

Jina la mtafiti: Hasanau Abduljabaar Ali Ali Akbaru – Iraq.

Tunapenda kusema kua; kongamano hili limefanywa kwa mwaka wa pili mfululizo, kutokana na Atabatu Abbasiyya tukufu kuamini kua jambo hili linaumuhimu na nafasi kubwa ya kutangaza utukufu wa bibi Zaharaa (a.s) na kubainisha dhulma kubwa aliyo fanyiwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: