Haya ndiyo maazimio ya washiriki wa kongamano la kielimu awamu ya pili kuhusu ukimbizi na uhamiaji…

Maoni katika picha
Washiriki wa kongamano la kielimu awamu ya pili kuhusu ukimbizi na uhamiaji, lililo simamiwa na chuo kikuu cha Alkafeel kwa kushirikiana na kitivo cha uuguzi / cha chuo kikuu cha Kufa, lililo isha ivi karibuni na kushiriki watafiti wa kisekula wa ndani na nje ya Iraq, wametoa maazimio yafuatayo:

  • 1- Kutilia umuhimu katika kuweka kumbukumbu ya juhudi zinazo fanywa na watumishi wa kusaidia wakimbizi wa kitaifa na kimataifa.
  • 2- Kuimarisha mawasiliano baina ya sekta tendaji, kama vile wizara ya afya, uhamiaji, ulinzi, mambo ya ndani, malezi, elimu ya juu na tafiti za kielimu na sekta zingine za kiserikali na kimataifa, kwa ajili ya kuwahudumia wakimbizi katika kambi zao za sasa na kuharakisha mpango wa kuwarudisha katika miji yao.
  • 3- Wizara ya mambo ya nje ifanye sense ya kutambua idadi halisi ya wahamiaji wa kiiraq, na sehemu wanazo patikana sambamba na kubaini hali zao za kimaisha, na kuwafatilia kwa karibu ili kulinda utukufu wao na haki zao za kuishi maisha bora.
  • 4- Kuwe na mpango wa kitaifa wa kuwalinda wakimbizi wa ndani, unao endana na sera zinazo simamia haki za binadamu na mikataba ya kimataifa.
  • 5- Kuandaa nadwa na warsha kwa watendaji wa kitaifa kwa ajili ya kuwajengea uwezo katika mambo ya kiofisi na namna ya kukabiliana na mazingira tofauti na kuhakikisha wanafanya juhudi na mipango ya pamoja.
  • 6- Kusoma misingi ya sheria zinazohusu uhamiaji na ukimbizi, kwa kufanya warsha na nadwa chini ya wataalamu ili kutoa mapendekezo ya kurekebisha au kuunda sheria zitakazo toa ufumbuzi wa tatizo la wahamiaji na wakimbizi katika siku zijazo.
  • 7- Kilipa kipawa mbele swala la kinafsi na kielimu kwa wakimbizi tena haraka, kwa kuwawekea mazingira bora ya kusomea na kuwafundisha uzalendo wa taifa lao la Iraq.
  • 8- Kuunda kamati itakayo kua na wajumbe kutoka katika chuo cha Alkafeel na kutoka katika kitivo cha uuguzi cha chuo kikuu cha Kufa kwa ajili ya kufuatilia maazimio tajwa hapo juu.

Kumbuka kua kongamano hili limefanyika kwa ajili ya kuangalia huduma za kijamii wanazo pewa wakimbizi wawapo ukimbizini, na kuangalia namna ya kutatua changamoto za kisheria zinazo husu kurudi kwa wakimbizi katika miji yao kwa hiyari, pamoja na kuimarisha ushirikiano wa sekta za serikali na zisizo kua za serikali za kitaifa na kimataifa katika kutoa huduma baada ya kipindi cha ukimbizi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: