Kimetolewa hivi karibuni na Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la wanawake: Athari za kutofautiana kwa Maswaadiq katika tafsiri ya Qur’an tukufu…

Maoni katika picha
Kimetolewa hivi karibuni na Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la wanawake, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kitabu cha: (Athari za kutofautiana kwa Maswaadiq katika Qur’an tukufu) kilicho andikwa na bibi Fatuma Muhammad Jawaad Habibu, na kuchapishwa na Darul-Kafeel chenye kurasa (414).

Toleo hili kwa mujibu wa maelezo ya muandishi wake: “Nimefuata njia ya Istiqraai Naqdiy katika maoni yenye utata na kuchanganya, nimefafanua mifano na kutaja tofauti za wanachuoni wafasiri katika jambo hilo, kisha nikaelezea sababu za kutofautiana kwao, pamoja na kuainisha mtazamo sahihi kwa kutumia dalili zinazo faa kupasisha, nikajaribu kukusanya maoni yanayo weza kukusanyika na kupunguza tofauti, au kuziweka mbali zinazo faa kuwekwa mbali, pia nimeelezea athari ya kua nyingi maswaadiq za Nasu”, akafafanua kua: “Utafiti wa sasa ulijikita katika misingi mikuu mitatu ambayo ni; utangulizi, tamhidi na ya mwisho ni hitimisho kwa kuangalia matokea muhimu, baada ya hapa mapokeo muhimu na vitabu rejea”.

Akaongeza kusema kua: “Kitabu hiki kina sehemu tatu, sehemu ya kwanza: Inazungumzia sababu za kutofautiana kwa maswaadiq, na inamada kuu tatu. Sehemu ya pili: Inazungumzia athari za kutofautiana kwa maswaadiq katika aya za Aqida, na inamada tano. Sehemu ya tatu: Inakamilisha sehemu ya pili, na imebeba jina la (Athari za kutofautiana maswaadiq katika aya za Ahkaami) na inamada nne”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: