Chuo kikuu cha Ameed chakaribisha mgeni muiraq dokta Alaa Habba kutoka chuo kikuu cha Watford cha USA…

Maoni katika picha
Kutokana na mkakati wa kunufaika na akili (ujuzi) wa wairaq wanao ishi nje ya nchi, na kuwatengenezea mazingira ya kurudi nchini kwao au kunufaika na ujuzi wao na kuufanyia kazi kwa vitendo katika taasisi za kisekula hapa Iraq, chuo kikuu cha Ameed chini ya uongozi wa malezi na elimu ya juu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umepata mgeni muiraq aishie ugaibuni, Dokta Alaa Habba kutoka chuo kikuu cha Watford cha USA.

Baada ya kutembelea sehemu za chuo na kuangalia selebasi ya masomo inayo tumika, alifurahishwa sana na mpangilio huu wa elimu utakao leta mafanikio makubwa katika elimu ya Iraq hapo baadae.

Katika ziara hii Dokta Alaa Habba alitoa muhadhara unao sema: (Utambuzi wa kiviwanda katika tiba ya sasa na ya baadae) mbele ya rais wa chuo Profesa Jaasim Marzuki na jopo kubwa la walimu na wanafunzi.

Kwa mujibu wa maelezo ya Dokta Alaa Habba: “Muhadhara wake ulichukua saa mbili na alielezea mada ya utambuzi wa kiviwanda katika tiba, hali kadhalika alielezea mambo mbalimbali na akatoa ufafanuzi muhimu kuhusu hali ya sasa na ya baadae katika utambuzi wa kiviwanda, pamoja na kufafanua misamiati muhimu ya kielimu inayo husu walimu wote wa chuo na wanafunzi wao, yenye ujumbe mkubwa unao saidia kukuza uzowefu kielimu na kivitendo”.

Akabainisha kua: “Hakika tunafanya kila tuwezalo kufikisha ujumbe muhimu wa elimu kwa wanafunzi wa chuo cha udaktari hadi katika siku za usoni, na aina ya tiba watakazo toa, kutokana na maendeleo ya kielimu na kiteknolojia katika sekta ya matibabu na vipimo, na upande wa kusoma na kusomesha, mtahitajia teknolojia kubwa na utendaji makini utakao akisi mafanikio ya kielimu na kivitendo”.

Kumbuka kua chuo kikuu cha Ameed ni moja ya taasisi muhimu za elimu zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kimefungua kitivo cha kwanza cha udaktari chenye kiwango cha kitaifa, na inatumia selebasi ya kimataifa, kwa ajili ya kuhakikisha inafikia viwango bora zaidi kila baada ya muda fulani hufanya kongamano au nadwa za kielimu ambapo hutolewa mihadhara mbalimbali na harakati zingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: